Tuesday, February 3, 2015

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AWASILI NCHINI.


Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa…



Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na msafara wake amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu majira ya saa 2.40.

Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt  amelakiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilali pia mapokezi ya burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na wananchi waliojitokeza kumpokea.

Rais huyo  ambaye anaitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia  mwaliko kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete atapata mapokezi rasmi kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.

Akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.

Pia Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha.

0 Responses to “RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AWASILI NCHINI.”

Post a Comment

More to Read