Friday, February 6, 2015
TANI 200,000 ZA SILAHA HARAMU ZATEKETEZWA.
Do you like this story?
TANI 200,000 za
silaha haramu zilizokuwa zimezagaa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) zimeteketezwa.
Hayo yalisemwa jana
na Katibu Mkuu wa EAC, Richard Sezibera mbele ya Rais
wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck wakati
alipozuru makao makuu ya jumuiya hiyo, jana.
Alisema silaha hizo
zilizokamatwa kwa nyakati tofauti katika nchi mbalimbali za EAC ni pamoja na
mabomu tani 200.
Akizungumzia ujio wa
Rais wa Ujermani katika makao makuu ya Jumuiya hiyo, Sezibera alikiri
kufurahishwa na ujio huo na kusema kuwa utaongeza chachu ya nchi hiyo kuisaidia
jumuiya hiyo.
Sezibera alisema
mahitaji makubwa yanahitajika katika kufanikisha mahitaji ya wananchi wa EAC
ikiwa ni pamoja na Afya, Mazingira, Miundombinu na vikundi vya akina mama na
vijana wanachama wa jumuiya hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “TANI 200,000 ZA SILAHA HARAMU ZATEKETEZWA.”
Post a Comment