Saturday, May 14, 2016
LHRC YAONYA KUHUSU PICHA ZA UCHI NA ZA KUTISHA
Do you like this story?
Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonya vitendo vinavyofanywa na baadhi
ya watu kuchapisha picha za utupu ama za kutisha katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam , Mkurungenzi Mtendaji wa
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo Bisimba alisema kuwa,
kumekuwa na matukio kadha yanayofanywa na watu juu ya kurekodi na kupiga picha
ambazo sio nzuri kwa mujibu wa sheria.
Alibainisha
picha hizo kuwa ni pamoja na matukio ya mauaji, ajali za kutisha na miili ya
marehemu zinazochapichwa katika mutandao ya kijamii, blog na hata baadhi ya
vyombo vya habari bila kijali kwamba, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Dk. Kijo
alisema kuwa, tarehe 4 Mei mwaka huu katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo
picha za miili ya marehemu (mama na mtoto) ambayo majina yao yamehifaziwa,
zilisambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha majeraha ya
kutisha kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa.
Katika
tukio la pili alibainisha kuwa, ilitokea Mkoa wa Kilimanjaro mwaka huu ambapo
picha za maiti ya mtoto aliyeuawa na mama wa kambo zilionesha akiwa ndani ya
jeneza.
Katika
maeneo ya Kibamba Jijini Dar es Salaam, Januari mwaka huu picha za utupu za
mwanamke aliyesemekana kuwa ni msukule aliyekutwa kwenya kisima zilizambazwa
katika mitandao ya kijamii.
Alisema
kuwa, hayo ni baadhi ya matukio hivyo jamii inapaswa kutambua kuwa vitendo
hivyo ni udhalilishaji na kinyume cha sheria.
“Kwani
kwa mujibu wa haki ya kikatiba ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya 1977 kila mtu ana haki ya kikatiba ya kuthamini utu wake kuwa
faragha akiwa hai au amefariki,”
alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LHRC YAONYA KUHUSU PICHA ZA UCHI NA ZA KUTISHA”
Post a Comment