Thursday, May 5, 2016
MMILIKI WA TIMU YA TP MAZEMBE ATANGAZA KUWANIA URAIS JAMHURI YA DEMOKRASIA YA CONGO
Do you like this story?
MOISE
Katumbi Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Mkurugenzi wa klabu ya TP Mazembe
na mfanyabiashara marufu nchini Kongo ametangaza kugombe urais wa Novemba mwaka
huu.
Muungano wa
vyama kadha vya upinzani umemuidhinisha Katumbi kuwa mgombea huku muungano huo
ukiwa umegubikwa na hofu ya huenda Rais Joseph Kabila akaendelea kushikiri
madaraka kinyume na katiba hiyo.
Katumbi
amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini ya chama cha People’s Party
for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae akajiuzulu nafasi hiyo
septemba 2015 ambapo mwaka huu 2016 amekuwa akitoa kauli zinazo mtaka Kabila
kuheshimu katiba ya taifa hilo inayo mtaka kustaafu mwishoni mwa mwaka huu.
Licha ya
Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011
kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo tangu kujiuzulu kwake 2015.
Hata hivyo
mfanyabiashara huyo amekuwa na umaarufu mkubwa kutokana na kumiliki klabu ya TP
Mazembe tangu 1997.
Uchaguzi
huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa Katumbi ana nguvu kubwa ya
kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na katika ngazi ya taifa licha ya
kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati wauongozi wake.
Wachunguzi
wa habari za siasa wamesema nchi hiyo inanyemelewa na machafuko iwapo Rais
Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa hilo kwa nguvu kama ilivyo fanyika
Burundi na Rais Nkurunzinza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MMILIKI WA TIMU YA TP MAZEMBE ATANGAZA KUWANIA URAIS JAMHURI YA DEMOKRASIA YA CONGO”
Post a Comment