Friday, March 13, 2015
MSAADA WATOLEWA MBEYA KWA ALBINO ALIYEKATWA KIGANJA SUMBAWANGA.
Do you like this story?
Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Rufaa Bw Ulusubisya Mpoki akimkabidhi Msaada mama mzazi wa Baraka Mara baada ya kumtembelea Hodini hapo |
Umoja wa wafanya kazi na wauguzi wa hospitali
ya Rufaa Mbeya pamoja na wananchi wamekabidhi msaada kwa mama wa mtoto
Baraka mlemavu wa ngozi (albino) aliyekatwa kiganja mkoani Rukwa
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Misaada
iliyotolewa na pesa tasilim shilingi laki nne, mavazi pamoja vyakula.
Akizungumza na waandishi wa habari wafanyakazi hao wameiomba serikali
kuchukua hatua kali kwa watu wanaowafanyia ukatili watu wenye ulemavu wa
ngozi maarufu kama maalbino ambazo zitaweza kukomesha ukatili huo
nchini Tanzania na kuhimiza kutendewa kazi kwa kauli mbiu ya 'MAUAJI YA
WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO) SASA IMETOSHA'
Pamoja na
hayo mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa Mbeya, ndugu Ulusubisya Mpoki
amewashukuru wananchi waliojitolea kutoa msaada wao wa hali na mali kwa
wahanga wa tukio hilo pamoja na wauguzi waliojitolea kumuuguza wahanga
mpaka sasa ambapo hali zao zinaridhisha.
Kufuatia
tukio hilo mama wa mtoto Baraka aliyejeruhiwa ametoa shukrani zake za
dhati kwa wote walioguswa na matatizo yao lakini pia mama huyo ambaye
kwa sasa ni mjamzito na anae mtoto mwingine mdogo ambaye pia yuko
hospitali ameonesha hofu ya kurudi kijijini kwake kutokana na balaa
lililompata mwishoni mwa wiki iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MSAADA WATOLEWA MBEYA KWA ALBINO ALIYEKATWA KIGANJA SUMBAWANGA.”
Post a Comment