Wednesday, April 15, 2015

ALICHOKISEMA MSANII WA FILAMU JACOB STEVEN 'JB' KUHUSU MBEYA CITY v SIMBA JUMAMOSI


JB (kulia) ni timu Simba wakati Ray (kushoto) ni timu Yanga


MSANII maarufu wa filamu nchini, Jacob Steven 'JB' amesema timu yake ya Simba itafanya vizuri dhidi ya Mbeya City fc katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayochezwa jumamosi ya wiki uwanja wa CCM Sokoine Mbeya.

"Nakumbuka vijana wa City ni wasumbufu, mwaka jana tulitoka 2-2 Taifa, tukaenda kwao tukatoka 1-1. Msimu huu mechi ya kwanza walitufunga 2-1 Taifa, sasa majeshi yetu yako fiti, lazima wakae"

"Naipenda sana Simba, namshukuru sana marehemu Babu yangu aliyenifanya niipende timu sahihi, kwingine utahangaika tu, Simba baba lao, tunasema Wekundu wa Msimbazi Simba, Taifa kubwa, Mnyama mkali! hahahahahah!"

JB ambaye hakosi kwenye mechi za uwanja wa Taifa anazocheza Simba sawa na mwenzake Vicent Kigosi 'Ray' anayeishabikia Yanga ameongeza kuwa timu yao imeyumba misimu mitatu mfululizo, lakini ni wakati wa mpito.

"Tumepitia misukosuko, lakini kocha kopunovic (Goran) anaonekana kuibadilisha timu, tunacheza soka safi, nina matumaini msimu ujao ubingwa utakuwa wetu, msimu huu mhhhhh! lazima tuwe wakweli, mambo magumu".
Simba wako nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu msimu huu wakijikusanyia pointi 35 katika mechi 21 walizoshuka dimbani.

0 Responses to “ALICHOKISEMA MSANII WA FILAMU JACOB STEVEN 'JB' KUHUSU MBEYA CITY v SIMBA JUMAMOSI”

Post a Comment

More to Read