Wednesday, April 15, 2015
RADI YASABABISHA TENA MAUAJI YA KUTISHA HUKO KIGOMA.
Do you like this story?
WATU wanane wakiwemo wanafunzi sita wa shule ya msingi
kibirizi Manispaa ya Kigoma wamekufa baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua
kubwa iliyonyesha.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa kigoma
Maweni,DK.FADHILI KIBAYA amesema sambamba na watu hao waliofariki pia
watu 15 wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Dk.Kibaya amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Yusuf
Athuman, Hassan Ally, Fatuma Sley, Zamda Seif, Shukrani Yohana na Warupe Kapupa
ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule hiyo ambapo Mwalim
aliyefariki ametambuliwa kwa jina la Elieza Mbwambo aliyekuwa akifundisha
darasa la tano.
Aidha pamoja na watu hao mtu mwingine aliyetambuliwa kwa
jina la Focas Ntahamba pia amefariki kwa kupigwa na radi katika eneo la Bangwe
mjini kigoma.
Mmoja wa walimu wa shule ya msingi ya kibirizi,WILBERT
EMANUEL ambaye alikuwepo eneo la tukio amesema kuwa wamesikitishwa na tukio
hilo ambalo lilitokea bila kutegemea na kuacha simanzi kubwa shuleni hapo.
Hili ni tukio la pili kutokea mkoani kigoma ambapo takriban
mwezi mmoja uliopita wanafunzi sita na mwalim wao walikufa
baada ya kupigwa na radi katika shule ya msingi nyakasanda katika kijiji cha
nyachenda wilayani kasulu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RADI YASABABISHA TENA MAUAJI YA KUTISHA HUKO KIGOMA.”
Post a Comment