Wednesday, April 15, 2015

AIBU! DEREVA WA SERIKALI ALEWA POMBE, AGONGA MTU NA GARI LA TCC MBEYA



Dereva George aliyesababisha ajali

Gari la TCC lililogongwa








Katika hali isiyo ya kawaida na isiyotegemewa dereva wa serikali aliyekuwa akiendesha gari la serikali aina ya Toyota Landcruiser la hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya jioni ya leo akiwa amelewa amegonga mtu mmoja na gari la TCC maeneo ya Uhindini katikati ya jiji la Mbeya.


Dereva huyo aliyefahamika kwa jina moja la George aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili STK 8248 mali ya serikali amefanya tukio hilo akiwa na watu wawili katika gari hilo, mwanamke na mwanaume ambao imeelezwa kuwa walitokea katika baa maarufu jijini Mbeya iitwayo Two Thousands (2000) walipokuwepo pamoja wote watatu wakilewa.

Tukio hilo limetokea wakati wakitoka katika baa hiyo ndipo akamgonga mwanamke mmoja katika njia panda ya kituo cha daladala cha Retco na alipofanya tukio hilo ndipo aliamua kukimbia kwa kuvunja masharti ya barabara inayoelekea hospitali ya Agha Khan kwani ni 'One-way' inayoteremka na si kupandisha na alipohamaki alikuwa tayari amegonga gari la Shirika la Sigara Tanzania (TCC) lenye namba za usajili T 840 BUU kulisababishia uharibifu ubavuni na kupasuka gurudumu la nyuma.

Hakuna madhara makubwa ya kibinadamu yaliyotokea katika ajali hiyo zaidi ya kusababisha maumivu ya mkono kwa mwanamke aliyegongwa ambaye aliwahishwa katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa. Mpaka Fichuo ikitoka katika eneo la tukio, dereva huyo alikuwa wamekwisha chukuliwa na jeshi la polisi pamoja na gari lililosababisha ajali hiyo kupelekwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Mbeya.

0 Responses to “AIBU! DEREVA WA SERIKALI ALEWA POMBE, AGONGA MTU NA GARI LA TCC MBEYA”

Post a Comment

More to Read