Tuesday, April 14, 2015
CHIKAWE ATOA TAMKO KUHUSU KURA YA MAONI NA UCHAGUZI MKUU.
Do you like this story?
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, akitoa tamko. |
Wanahabari wakimfuatilia Chikawe. |
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe, ametoa tamko kuhusu mustakabali wa nchi
kuelekea zoezi la kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu ujao
na namna matukio mengi yanavyoweza kuibuka na kuashiria uvunjifu wa amani
nchini.
Akizungumza na wanahabari wizarani kwake leo,
Chikawe alisema kuwa kila inapofika wakati wa kuelekea chaguzi
mbalimbali, kumekuwa kukitokea matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani
yanayofanywa na watu ama vikundi vya watu.
Alisema matukio hayo yamekuwa yakisababishwa
na hamasa za kisiasa au baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia muda huu
kutekeleza ajenda zao za kihalifu kwa kisingizio cha vuguvugu za kisiasa au
yote mawili.
Alivitaka vyama vya kisiasa kuepuka kufanya
ushabiki wa kubeba wanachama wao kutoka sehemu moja kwenda sehemu
nyingine wakati wanapoandaa mikutano yao na badala yake wawashirikishe
wanachama waliopo katika sehemu wanapotaka kufanyia mikutano hiyo.
Chikawe amesema hivi karibuni kumekuwa na
matukio yanayotokana na baadhi ya viongozi wa taasisi za dini kutoa
matamko ambayo yanaashiria kuingilia masuala ya kisiasa kinyume cha sheria ya
vyama , sura ya 337 na kanuni zake pamoja na katiba zinazosimamia uendeshaji wa
taasisi hizo.
Alitoa mifano ya viongozi wa taasisi za dini
wanapokutana na kutoa matamko yanayolenga kuwashawishi waumini wao wafuate
maelekezo yao kuhusiana na masuala ya Katiba Inayopendekezwa au kuhusu uchaguzi
mkuu ujao,
matamshi ambayo yanakiuka sheria ya usajili wa taasisi hizo.
‘’Ni kweli kuwa viongozi hao wa dini wana
haki ya kushiriki katika masuala ya kisiasa kama watu binafsi ila ni
kinyume cha sheria kutumia uongozi wao kuwashawishi waumini wao watekeleze
matakwa yao ya kisiasa,’’ alisema Chikawe.
Alisisitiza kuwa serikali itachukua hatua
kali kwa watu binafsi, vyama vya siasa na taasisi za kidini zitakazobainika kuvuruga
usalama na utulivu wa nchi, ikiwa ni pamoja na kufuta usajili wa vyama vya
kijamii na vya kidini ambavyo vitakiuka katiba ya kuanzishwa kwao.
HABARI/PICHA NA DENIS MTIMA/GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHIKAWE ATOA TAMKO KUHUSU KURA YA MAONI NA UCHAGUZI MKUU.”
Post a Comment