Wednesday, April 15, 2015
WALIOFARIKI KWA RADI MKOANI KIGOMA WAAGWA.
Do you like this story?
Miili ya wanafunzi sita, Mwalimu mmoja na mkazi wa eneo la Bangwe ikiwa tayari kwa kuagwa katika viwanja vya shule ya Msingi Kibirizi mkoani Kigoma. |
Watu wanane wakiwemo wanafunzi sita wa shule
ya msingi Kibirizi, mwalimu mmoja pamoja mkazi wa eneo la Bangwe mjini hapo
walipoteza maisha hapo jana baada ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengine 15
wakijeruhiwa na radi hiyo.
Miili ya marehemu imeagwa mchana huu wa leo
katika viwanja vya Shule ya Msingi kibirizi tayari kwa mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu Issa
Machibya alihudhuria katika shughuli hiyo ya kuwaaga marehemu wanjani hapo na
kutoa salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa za wafiwa.
kwa upande wake, Katibu wa Bakwata mkoa wa
Kigoma, Shekhe Moshi Guoguo alitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na Taifa kwa
ujumla, aliwataka waombolezaji kuwa wapole na wavumilivu hasa katika wakati huu
mgumu wa majonzi ya kupotelewa na ndugu zao wapendwa.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA
LIHIMIDIWE!
CHANZO: MICHUZI BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIOFARIKI KWA RADI MKOANI KIGOMA WAAGWA.”
Post a Comment