Wednesday, April 15, 2015
POLISI: MADEREVA WOTE WALIOSABABISHA AJALI KWA UZEMBE ZIKIWEMO ZA HIVI KARIBUNI WATAFUTIWA LESENI ZAO .
Do you like this story?
KIKOSI
cha Usalama Barabarani nchini, kimesema madereva wote waliosababisha ajali kwa
uzembe zikiwemo za hivi karibuni, watafutiwa leseni zao.
Kamanda wa kikosi hicho, Mohamed Mpinga, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa, ili kukabiliana na wimbi la ajali jeshi hilo limeazimia kufuta leseni za madereva hao.
Alisema ajali za hivi karibuni, zimesababishwa na uzembe wa madereva; hivyo ni lazima wafutiwe leseni na hawapaswi kufanya kazi ya udereva nchini na taarifa zao zitawekwa kwenye tovuti ili waajiri wengine wasiwachukue.
"Kuanzia sasa, mabasi yote yaendayo mikoani tutakuwa tunaangalia yametoka kituoni saa ngapi kwenye maeneo mbalimbali hadi linapomaliza safari yake...likiwa mbele ya muda hatua stahiki zitachukuliwa," alisema.
Kamanda Mpinga ametoa pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali za hivi karibuni.
CHANZO : GAZETI LA MWANANCHI

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI: MADEREVA WOTE WALIOSABABISHA AJALI KWA UZEMBE ZIKIWEMO ZA HIVI KARIBUNI WATAFUTIWA LESENI ZAO .”
Post a Comment