Wednesday, April 15, 2015
MCHEZAJI WA ZAMANI WA KMKM NA TIMU YA TAIFA. MCHA KHAMIS AFARIKI DUNIA.
Do you like this story?
Marehemu Mcha Khamis Mcha. |
Buriani
Mchezaji wa Zamani wa timu ya KMKM na Miembeni Zanzibar Mcha Khamis Mcha
aliyefarika jana Mjini Dar-es-Salaam akipata matibabu katika hospitali ya
Muimbili. kwa mujibu wa habari za ndugu wa karibu wamesema alikuwa akisumbulia
na matatizo ya mkojo.
Mwili
wa marehemu unatarajiwa kuwasili Zanzibar leo katika bandari ya Malindi saa.6
mchana kwa Boti ya Azam Marine, baada ya kuwasili mwili wa marehemu utapelekwa
Kijiji kwao Mkwajuni Unguja, kwa mazisha leo baada ya sala ya alasiri.
Marehemu Mcha Khamis Mcha amejiunga na timu ya KMKM katika mwaka 1978, baada ya kumaliza masomo yake, Mcha Khamis alichezea timu za Taifa ya Zanzibar na Timu ya Taifa Stars ya Tanzania kwa vipindi tafauti.
CHANZO>DAR ES SALAAM YETU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MCHEZAJI WA ZAMANI WA KMKM NA TIMU YA TAIFA. MCHA KHAMIS AFARIKI DUNIA.”
Post a Comment