Thursday, July 23, 2015
DAR WAFURIKA KWENYE VITUO VYA KUJIANDIKISHA BVR
Do you like this story?
MAELFU
ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, jana walijitokeza kwa wingi katika siku ya
kwanza ya uandikishaji wapigakura katika mfumo wa kisasa wa kielektroniki
(BVR), licha ya kuwapo kwa changamoto kadhaa.
Katika
vituo vingi, licha ya wananchi kujitokeza kuanzia mapema alfajiri, changamoto
kadhaa zilijitokeza, ikiwemo mashine kushindwa kufanya kazi kutokana na
hitilafu, hivyo kuchelewesha uandikishaji, ingawa baadaye ufumbuzi ulipatikana.
Wachangishana
pesa
Katika
Kituo cha Shule ya Msingi Tabata Kisukuru, Manispaa ya Ilala, licha ya kituo
kuwa na mashine mbili, zote zilishindwa kuwaka kutokana na kutokuwa na umeme
huku kifaa cha umemejua kikielezwa kuwa na hitilafu.
Kutokana
na hali hiyo, wananchi walihamasishana kuchanga Sh 100 kila mmoja ili kupata Sh
30,000 za kulipia umeme uliokuwa umeombwa na watumishi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kutoka nyumba ya jirani.
Baada
ya mjadala, baadhi ya wananchi hao waliofikia 800 waligoma kulipa wakidai
Serikali ilishatenga fedha za uandikishaji wapigakura. Hali hiyo ilisababisha
kuchelewa zaidi kwa kazi ya kuandikisha wapigakura.
Pamoja
na kuchelewa huko, baadhi ya wananchi hawakukata tamaa, mpaka alipokuja ofisa
mwingine wa tume aliyetengeneza vifaa vya umeme jua na ndipo uandikishaji
ukaanza majira ya saa saba.
Wachezeana
rafu
Wakati
wakisubiri kuandikishwa, baadhi ya wananchi walijikuta wakitafuta mbinu ya
kuwahi kuandikishwa, kwa kughushi namba zao, mathalani, aliyekuwa kwenye nafasi
ya 300 na kupewa namba 300, alifuta sifuri moja ili isomeke 30.
Kuna
waliofanikiwa, lakini wengine walikwama kutokana na kutumia wino tofauti na ule
ulioandikwa katika karatasi za awali na wahusika. Pugu ‘ngoma’ yalala Katika
kituo cha Pugu Stesheni, wananchi wapatao 500 waliowahi katika kituo hicho
kujiandikisha, walitakiwa kurudi nyumbani na kurejea leo kutokana na mashine
kusumbua na kuwa itaandikisha watu 10.
Kituo
cha Mistuni A na B kulikuwa na misururu kutokana na kazi ya uandikishaji
kutoanza kutokana na ubovu wa vifaa.
Mpaka
HabariLeo inafika kwenye vituo hivyo viwili majira ya saa 6 mchana, hakuna
mwananchi yeyote aliyeandikishwa kutokana na mashine ya kituo cha Mistuni A
kusumbua kamera huku Mistuni B mashine ya kuchapa karatasi kukorofisha.
“Mpaka
sasa bado hatujaanza kuandikisha, mashine moja kamera inasumbua, na mashine
nyingine inasumbua na ndio mafundi wanahangaika kutengeneza. Muda wowote
mashine zitakapotengamaa basi tutaanza kuandikisha,” alisema ofisa wa tume
ambaye alikataa kutaja jina lake.
Katika
kituo cha uandikishaji cha Majengo Vingunguti, umati wa
watu wakizozana wakiwa kwenye mstari, hali ambayo imechangiwa na kuchelewa
kuanza kwa kazi hiyo.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mitaa wa Majengo Vingunguti, Chande Msoke alisema kumekuwapo na
tatizo la kuchelewa kwa vifaa, jambo ambalo limefanya kazi hiyo ianze kwa
kuchelewa saa tatu, jambo ambalo limesababisha mizozo ya hapa na pale.
“Watu
wamefika hapa saa 11: 30 asubuhi, vifaa na ufungaji wa turubai umechelewa jambo
ambalo limesababisha vurugu za hapa na pale. Tulichofanya tuliwaandikisha wale
waliofika mapema na pale kazi ya uandikishaji ilipoanza ndio walioanza
kuhudumiwa. Aliongeza: “Kutokana na kuchelewa kuanza watu wamekuwa wakali kiasi
ambacho hata akija mama mjamzito, mzee au mlemavu wanakataa kumpisha, haya yote
yanachangiwa na kuchelewa jambo ambalo linafanya watu kukaa sana kituoni.
Kuhusu
kasi ya kuandikisha, Msoke alisema imekuwa ikienda taratibu kutokana na mashine
kushindwa kutambua alama za vidole kwa baadhi ya watu ambao inawachukua dakika
45 kukamilisha kazi hiyo.
“Wale
ambao mashine inashindwa kutambua alama za vidole, tunawataka wakanawe mikono
na sabuni, na kama bado itakuwa shida, basi tunamtaka arejee kesho,” alisema.
Katika
kutuo cha Mchafukoge, Mnazi Mmoja, kazi ya uandikishaji ilichelewa na ilianza
saa 3 asubuhi kutokana na kuchelewa kufikishwa vifaa huku kazi hiyo ikifanyika
taratibu sana.
Katika
kituo cha Majani ya Chai, Kipawa, shughuli ya uandikishaji ilianza saa tatu
asubuhi na baada ya kuhudumia watu watano mashine ilikorofisha hivyo kufanya
kazi hiyo kusimama kwa muda.
Ubungo
yale yale
Wakati
hayo yakitokea katika Manispaa ya Ilala, katika wilaya ya Kinondoni nako
uandikishaji ulianza kwa kusuasua, licha ya wananchi kujitokeza kwa wingi.
Ilielezwa uchelewaji huo ulitokana na mashine hizo kuletwa juzi usiku na hivyo
kazi ya ufungaji kuchelewa, ikielezwa kila kituo kina mtaalamu mmoja wa
teknolojia ya habari na mawasiliano (IT).
Katika
kituo cha kujiandikisha cha shule ya msingi Ubungo Plaza, Mwandishi Msaidizi wa
kituo hicho, Charles Samson akiwa na wenzake wawili, walionekana kukaa bila
kufanya jambo lolote huku amezongwa na watu na kusema mashine hizo zilipokelewa
juzi usiku, hivyo hazijawekewa software.
Alisema
hatua hiyo inatokana na kuwa mtaalamu wa IT kutoka NEC kuwa mmoja katika kata
hiyo ya Ubungo, hivyo walimsubiri hadi alipokamilisha kazi na uandikishaji
kuanza baada ya saa nne. Aidha, ilielezwa baadhi ya watu waliokuwa na haraka za
kuendelea na shughuli zao, walishindwa kusubiri wakiahidi kurudi baada ya mambo
kuwa sawa.
Nako Mbezi
Beach katika eneo la Miti Mirefu mpaka kufikisha saa nne asubuhi uandikishaji
ulikuwa haujaanza kutokana na kuwa vifaa hivyo vilikuwa havijafika, jambo
lililofanya watu kuondoka katika vituo huku wengine wakibaki na kupigwa na jua.
Huku
eneo la kawe walichelewa kuanza uandikishaji licha ya vifaa hivyo kuwa vimefika
kutokana na kudaiwa kuwa umeme ni mdogo hivyo mashine hizo hazikuweza kufanya
kazi mpaka kufikia saa nne asubuhi.
Temeke
nao wachelewa Kama ilivyokuwa Ilala na Kinondoni, wakazi wa Temeke nao
walijitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali vya uandikishaji, huku
changamoto ikiwa vifaa, ingawa baadaye ilipatiwa ufumbuzi.
Katika
kituo cha Mtaa wa Mwembebamia kata ya Chamazi, baadhi ya watu wananchi
waliojitokeza kujiandikisha walililamikia ucheleweshwaji uliofanywa na
waandikishaji hao kwani hadi kufikia saa 3 asubuhi uandikishaji ulikuwa bado
haujaanza.
Wakizungumza
na gazeti hili, walidai kuwa walifika mapema katika kituo hicho kwa matarajio
kuwa waandikishaji hao wangefuata ratiba na kuanza saa 2 ili waweze kuwahi
katika shughuli zao zingine.
Ramadhani
Issa, mkazi wa Mwembebamia B, alidai licha ya utaratibu wa kutoa namba kwa kila
mwananchi anayefika kuwa mzuri, lakini utaratibu huo una dosari kubwa kwani
baadhi ya watu walifika mapema lakini walipewa namba za mwishoni tofauti na
waliochelewa, suala linaloonekana kuwa ni kama kuna upendeleo.
Katika
Kata ya Maganga iliyopo Temeke watu waliojitokeza na walilalamikia
waandikishaji kwenda taratibu kutokana na mashine kuchelewa kufanya kazi, huku
mtu mmoja akilazimika kutumia hadi dakika 20 ili kupiga picha. Kwa upande wa
kata ya Azimio, watu wengi pia walijitokeza huku changamoto ya kuchelewa kufika
kwa wahusika na mashine kuwa chache.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ DAR WAFURIKA KWENYE VITUO VYA KUJIANDIKISHA BVR”
Post a Comment