Thursday, July 23, 2015

WARWANDA, WARUNDI KUTUNISHIANA MISULI LEO KAGAME, NIMEKUWEKEA RATIBA....




Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam inaendelea leo katika uwanja wa Taifa.

Majira ya saa 10:00 jioni,  Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR SC kutoka Rwanda wanacheza na LLB ya Burundi. 

Mchezo wa mapema utazikutanisha timu ya Heegan FC ya Somalia na Al Shandy ya Sudan.

Katika matokeo ya jana uwanja wa Taifa, mabingwa wa Tanzania bara, Young Africans waliibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Telecom kutoka nchini Djibout.

 Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu aliyefunga mabao mawili, na Geofrey Mwashiuya  aliyefunga bao la tatu kwa kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom. 

Hata hivyo,  Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake Amissi Tambwe na Saimon Msuva zilizookolewa na mlinda mlango wa Telecom,  Nzokira Jeef.

 Katika mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.

0 Responses to “WARWANDA, WARUNDI KUTUNISHIANA MISULI LEO KAGAME, NIMEKUWEKEA RATIBA....”

Post a Comment

More to Read