Sunday, July 12, 2015
MAGUFULI NDIYE MGOMBEA URAIS WA CCM 2015.
Do you like this story?
MBUNGE wa Biharamulo
Mashariki (CCM) na Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli ameshinda katika
uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda
baada ya kupata jumla ya kura 2104 sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali
amepata kura 253 sawa na 10.5% na Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ndiye aliyepewa jukumu la
kutangaza mshindi aliyepatikana kwa kura za Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM
kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi mkoani Dodoma.
KURA ZILIZOPIGWA:
2422
KURA ZILIZOHARIBIKA: 6
KURA HALALI: 2416
KURA ZILIZOHARIBIKA: 6
KURA HALALI: 2416
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAGUFULI NDIYE MGOMBEA URAIS WA CCM 2015.”
Post a Comment