Tuesday, September 1, 2015
.WAGOMBEA 38 WA NAFASI ZA UBUNGE WALIOWEKEWA PINGAMIZI KUENDELEA NA KAMPENI.
Do you like this story?
Na Anitha Jonas – MAELEZO.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini imefuta rufaa 38
za wagombea nafasi za ubunge kati ya 54 zilizowasilishwa kupinga baadhi ya
wagombea hao kwa kuwatuhumu kutotimiza vigezo mbalimbali na kusema wagombea hao
wanaweza kuendelea na Kampeni majimboni mwao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa
Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhan kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa baada ya Wakurugenzi wanaoshughulikia uchaguzi kuzipitia
,waligundua kuwa rufaa hizo waliziona hazina mantiki na kukosa ushahidi wa
kutosha.
“Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa katika uchaguzi ni
16 na Tume imewarudisha wagombea 13 kati ya hao na waliobaki watatu ,Tume
imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa Uchaguzi”,alisema Bw.Ramadhani.
Aliongeza kuwa Tume hiyo inaendelea kupitia rufaa za wabunge
zilizobaki kwa kushirikiana na wasimamizi wa uchaguzi ili
kupata vielelezo vinavyohusika na pindi itakapokamilisha zoezi hilo
itatoa taarifa yake ikiwa ni pamoja na rufaa 198 za madiwani kutoka
halmashauri mbalimbali nchini.
Aidha alisema kuwa Tume hiyo itaendelea kusimamia
haki na kufanya maamuzi ya kuzingatia sheria kwa wagombea wa vyama vyote
vilivyoshiriki katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwataka kuwa na imani na kazi
inayofanywa na Tume katika rufaa hizo.
Mbali na hayo Mkurugenzi wa uchaguzi alisema
kuwa Tume inatarajia kuanza zoezi la uhakiki wa daftari la mpiga
kura visiwani Zanzibar kuanzia tarehe keshokuwa (03/09/2015) ambapo zoezi hilo
litadumu kwa muda wa siku saba.
Akiongelea juu ya uhakiki wa taarifa za mpiga
kura aliyejiandikisha alisema unaweza kuhakiki taarifa zako kwa
kupitia mtandao wa tume www.nec.go.tz au kwa kupiga
*152*00// katika simu na kupata taarifa zote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “.WAGOMBEA 38 WA NAFASI ZA UBUNGE WALIOWEKEWA PINGAMIZI KUENDELEA NA KAMPENI.”
Post a Comment