Wednesday, September 2, 2015
TAKUKURU WAMBURUZA TENA HAKIMU MAHAKAMANI KWA MARA YA PILI.
Do you like this story?
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru) kwa mara nyingine imemtia mbaroni na kumfikisha
mahakamani aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, Oscar Bulugu,
kujibu mashtaka ya kuficha nyaraka za serikali na wizi wa majalada 31 ya kesi.
Mshtakiwa huyo alifikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Tabora mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emmanuel Ngigwana.
Mawakili Simon Mashingia na Edson
Mapalala, walidai kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Aprili 15 na
Novemba 11, mwaka 2013, mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo.
Ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,
mshtakiwa huyo akiwa mtumishi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
idara ya mahakama, aliiba majalada hayo ya kesi zilizokuwa zikiendelea
kusikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Urambo na kuyaficha nyumbani kwake.
Iliendelea kudaiwa kuwa mshtakiwa huyo
alitenda makosa hayo wakati akiwa amesimamishwa kazi na mwajiri wake kutokana
na kukabiliwa na kesi tatu za kuomba na kupokea rushwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora.
Awali Bulugu alifikishwa mahakamani
hapo mwaka 2013 na Takukuru akikabiliwa na mashtaka ya kuomba rushwa na kupokea
rushwa kati ya Machi 15 hadi 22, mwaka jana, akiwa hakimu mkazi wa wilaya
ya Urambo.
Ilidaiwa Machi 15 mwaka juzi, akiwa
hakimu wa mahakama hiyo, alimshawishi Lucas Changala ampatie rushwa ya
Sh. milioni 5 ili atoe dhamana kwa ndugu yake aliyekuwa anakabiliwa na
kesi ya wizi wa fedha za Benki ya NMB.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAKUKURU WAMBURUZA TENA HAKIMU MAHAKAMANI KWA MARA YA PILI.”
Post a Comment