Wednesday, September 2, 2015
ASKARI WANYAMA PORI WADAIWA KUWAPIGA WAFUGAJI NGORONGORO.
Do you like this story?
MGOGORO
mpya umeibuka Ngorongoro baada ya Askari wa Wanyamapori wa Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro kudaiwa kuwapiga wafugaji wa kata za Endulen na Alaitole
wanaoishi pembezoni mwa hifadhi hiyo.
Chanzo
cha mgogoro huo kinaelezwa kusababishwa na baadhi ya wafugaji kupeleka mifugo
yao eneo la Mash ambalo hutumiwa kunywesha mifugo yao hasa kipindi cha
kiangazi, ambapo askari walipowakuta walianza kuwashambulia kwa madai kuwa
hawaruhusiwi kufuga mifugo yao katika eneo hilo.
Wafugaji
hao wameeleza kuwa katika kipindi hiki cha kiangazi ambacho wanakabiliwa na
uhaba wa maji hasa kwa ajili ya mifugo yao na wamekuwa na utaratibu wa kutumia
eneo hilo kwa makubaliano ya kila mwaka ila kwa mwaka huu imekua tofauti kwani
wamefukuzwa pamoja na kupigwa na askari hao kinyume cha sheria.
Mzee
wa mila jamii ya Wamasai, Kadogo Olduati amesema kuwa kwa kipindi kirefu
wameishi katika ardhi mseto yenye mchanganyiko wa wanyamapori na mifugo pamoja
na binadamu bila kusababisha athari zozote katika kwa mazingira na wanyama.
Olduati
ameitaka Mamlaka ya Ngorongoro isiegemee upande wa wanyamapori na kuwasahau
wafugaji ambao hutegemea ufugaji kuendesha maisha yao ya kila siku.
Katibu
wa Baraza la Wafugaji, James Moringe ameiomba mamlaka ya Ngorongoro na Baraza
la wafugaji kwa pamoja kuitisha kikao cha haraka ili kuepusha mgogoro huo ambao
unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na kuathiri uhifadhi na utalii kwa
ujumla.
Mhifadhi
wa Ngorongoro hakuweza kupatikana kuzungumzia tikio hilo kwa kuwa simu yake ya
mkononi haikupatikana, lakini pia walinzi waliwazuia waandishi kuingia ofisini
kwake mpaka watakapopata kibali maalum.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ASKARI WANYAMA PORI WADAIWA KUWAPIGA WAFUGAJI NGORONGORO.”
Post a Comment