Saturday, October 17, 2015
KAULI YA KUUMIZA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Do you like this story?
Jioni ya jana,
Oktoba 15, helikopta namba 5Y-DKK ilipata ajali katika eneo lisilofikika
kirahisi (remote) la mbuga ya wanyama ya Selous, ikitokea Dar Es Salaam kwenda
Ludewa. Vyombo vya serikali (Wizara ya Maliasili na Utalii, TCAA, Polisi)
pamoja na kampuni binafsi za usafiri wa anga wameshirikiana usiku kucha kufika
eneo hilo.
Katika ajali hii Ndugu Deo Haule Filikunjombe
(Mbunge wa Ludewa) na Kapteni William Silaa pamoja na watu wengine wawili
wamefariki dunia. Chama na nchi imepoteza kijana makini, kiongozi bora, tegemeo
la wana Ludewa na mfano imara kwa vijana wa Tanzania. Familia ya Kapteni
William Silaa imepoteza baba, nchi imepoteza rubani mzuri. Tunaungana na
familia zote katika kipindi hiki kigumu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ KAULI YA KUUMIZA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)”
Post a Comment