Saturday, October 17, 2015
LOWASSA NAYE NA MSIBA WA DEO FILIKUNJOMBE.
Do you like this story?
"Ni taarifa ya
kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri, Deo Filikunjombe
kutokana na ajali ya Helikopta jana jioni maeneo ya mbunga ya Selous mkoani
Morogoro.
Ni pigo lingine kubwa
ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa na kidonda cha
kuondokewa na wana siasa wengine mahiri,Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah
Kigoda na Dr Emanuel Makaidi aliyefariki jana
Filikonjombe alikuwa
Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa jimbo lake la
Ludewa na watanzania kwa ujumla.
Alikuwa mwiba kwa
serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni katika kashfa ya
Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati iliyochunguza kashfa hiyo.
Mwenyezimungu awape
moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa Ludewa, katika kipindi
hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
BWANA AMETOA, BWANA
AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE," Edward Ngoyai Lowassa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ LOWASSA NAYE NA MSIBA WA DEO FILIKUNJOMBE.”
Post a Comment