Monday, December 7, 2015
UBUNGE WA SAED KUBENEA WAPIGWA MAHAKAMANI
Do you like this story?
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea. |
Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Massaburi. |
Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Massaburi, amefungua kesi ya kupinga ushindi wa
Saed Kubenea, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Dk. Massaburi
amefungua kesi hiyo ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mbali ya
Kubenea, wengine waliounganishwa katika kesi hiyo ni Masimamizi wa Uchaguzi
katika jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika kesi
hiyo, Dk. Massaburi anadai kwamba mshtakiwa wa kwanza (Kubenea), alitoa rushwa
ya kununua jenereta katika hospitali ya Mavurunza iliyopo kata ya Kimara, kutoa
rushwa ya ujenzi wa barabara ya Matete, kutoa zawadi kwa kununulia ‘Pool
Table’, kwa ajili ya kuwashawishi wananchi wampigie kura.
Madai dhidi ya
Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo ni hakumpatia nafasi ya kuhesabu kura upya
kama alivyoomba, hakumjulisha tarehe, muda na wapi matokeo ya jimbo hilo
yalikuwa yanajumulishwa, yeye na mawakala wake hawakuona wakati vifaa vya
uchaguzi vinafunguliwa.
Pia anadai
kwamba baadhi ya vituo havikufanya uchaguzi, na pia baadhi ya wapigakura
walipiga kura wakati hawajafikisha umri wa kupiga kura.
Katika madai
hayo, Dk. Massaburi anaiomba Mahakama Kuu itengue ushindi wa Kubenea
uliotangazwa na Msimamzi wa Jimbo hilo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Kubenea alithibitisha kupokea madai hayo kutoka kwa
Dk. Massaburi na kwamba ameombwa kuwasilisha utetezi wake katika mahakama hiyo
ndani ya siku 21.
Aidha, Kubenea
alisema katika kesi hiyo, atawakilishwa na jopo la mawakili watano akiwamo
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, Mabere Marando, Peter Kibatala,
Method Kimongoro na Frederick Kihwelo na kwamba wamepanga kuwasilisha utetezi
wao ndani ya wiki hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UBUNGE WA SAED KUBENEA WAPIGWA MAHAKAMANI”
Post a Comment