Wednesday, January 27, 2016
SIMBA ITACHUKUA UBINGWA WA VPL? HAYA NDIYO MAJIBU YA HAJI MANARA
Do you like this story?
Baada ya kikosi cha Simba kumaliza raundi ya
kwanza kikiwa nyuma ya vinara wa ligi kwa pointi sita, bado wanauota ubingwa wa
ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kutua kwa kocha Jackson Mayanja
ambaye kwa sasa anakinoa kikosi hicho baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha
mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr.
Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara
amesema, mikakati iliyopo sasa ni kuhakikisha Simba inapata matokeo mazuri
ambayo wanauhakika yataendelea kuwafanya wapambane na wapinzani wao kwenye
kinyang’anyiro cha ubingwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
“Tunaingia katika raundi ya lala salama
tukiwa na mtazamo positive kwamba tunazo chances za kuchukua ubingwa, kwa
hesabu zilivyo, tumezidiwa pointi sita na wapinzani wetu. Pointi sita ni maana
ya michezo miwili, kuna michezo 15 inakuja ya ligi kuu. Kwahiyo uongozi mzima
wa klabu ya Simba, benchi la ufundi na wachezaji focus yao ni kuchukua
ubingwa”, amesema Manara.
“Tunajua ligi ni ngumu hakuna mechi nyepesi
lakini tunaamini bado tunao uwezo mkubwa wa kuchukua ubingwa kutokana na
maboresho ambayo yamefanywa katika kikosi cha Simba hususan katika benchi la
ufundi baada ya kuingia mwalimu Jackson Mayanja, tunaona kuna kitu kinakuja
kile ambacho mashabiki wa Simba wanaona tunakikosa”.
Raundi ya kwanza imemalizika huku kikosi cha
Simba kikiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kikiwa na pointi 33
nyuma ya Yanga na Azam zenye pointi 39 lakini Yanga inakaa kileleni kutokana na
tofauti ya magoli dhidi ya Azam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA ITACHUKUA UBINGWA WA VPL? HAYA NDIYO MAJIBU YA HAJI MANARA”
Post a Comment