Wednesday, January 27, 2016
BAADA YA KUZAWADIWA KIWANJA KIGAMBONI, WASANII WAMFANYIA SAMATTA BONGE LA SURPRISE
Do you like this story?
Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeamua
kumpa uanachama wa heshima mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta pamoja na
kumzawadia ekari tano za ardhi katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga kwa
ajili ya kuanzisha Chuo cha Mafunzo ya soka.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema
jana kuwa kikao cha Kamati ya Utendaji ya Mtandao huo kilichoketi juzi
kilifikia uamuzi huo baada ya kufuatilia kwa karibu mafanikio ya Samatta akiwa
na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kongo na
kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika hadi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora
Afrika.
Alisema SHIWATA inatoa kiwanja hicho kama
zawadi kwa mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kulitangaza taifa katika
medani ya kimataifa katika mchezo wa soka ambako wengine watafuata nyayo zake.
Taalib alisema taratibu za makabidhiano
zinafanywa kwa mawasiliano na baba yake mzazi, Ali Samatta na atakabidhiwa eneo
hilo mara baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ambako anakwenda kusaini mkataba na
timu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji wa miaka minne.
SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000
inamiliki ekari 300 za kujenga makazi, kumbi za starehe, viwanja vya michezo na
nyumba za kuishi katika kijiji cha Mwanzega wilayani Mkuranga na ekari 500 eneo
la Ngarambe kwa ajili ya kilimo.
Wakati huo huo wasanii wanne maarufu nchini
wakiongozwa na Ahmed Olotu ‘Chilo’ juzi walinogesha tamasha la sanaa na michezo
wilayani Mkuranga walipoalikwa kuona sanaa inavyochezwa na wasanii wa wilaya
hiyo.
Mzee Chilo aliyefuatana na Boniface Mwanza
Mpango ‘King Kikii’, Wasanii wa Bongo Movie, Suzan Lewis ‘Natasha, Kulwa
Kikumba ‘Dude’ na Asha Salvador walijikuta wakishangiliwa mara kwa mara na
wasanii wenyeji ambao pia walipiga nao picha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BAADA YA KUZAWADIWA KIWANJA KIGAMBONI, WASANII WAMFANYIA SAMATTA BONGE LA SURPRISE”
Post a Comment