Wednesday, January 27, 2016
LUIS SUAREZ: “NITARUDI ENGLAND, KWA AJILI YA LIVERPOOL.
Do you like this story?
Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Luis Suarez
amezungumzia uwezekano wa yeye kurudi nchini England na kuichezea klabu yake ya
zamani ya Liverpool, huku akisema kuwa ndio klabu pekee anayoweza kurudi
England kwa ajili yake.
Suarez ambaye aliichezea Liverpool kwa kipindi
cha miaka 2 na nusu kabla ya kusajiliwa na Barcelona ya nchini Hispania
ameiambia ESPN kuwa kila mchezaji ambaye alipata kuichezea Liverpool anajua
umuhimu wa mashabiki wa Liverpool Anfield.
Suarez anasema kuwa mashabiki wa Liverpool ni
wa pekee zaidi duniani, na kwamba anawakumbuka kila wakati kitu kinachomfanya
awe na ndoto za siku moja kurudi tena Merseyside kufurahia tena maisha na
mashabiki hao.
Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax alijiunga
Liverpool mwaka 2011 kwa ada ya uamisho wa pauni 22m na katika kipindi cha
miaka 2 na nusu aliifungia Liverpool magoli 94 kabla ya kusajiliwa na Barcelona
kwa dau kubwa la pauni 75m.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ LUIS SUAREZ: “NITARUDI ENGLAND, KWA AJILI YA LIVERPOOL.”
Post a Comment