Wednesday, January 27, 2016
HOFU YA KUENEA KWA KIPINDUPINDU YATANDA KIGOMA
Do you like this story?
Na Emmanuel Senny, Kigoma
Wananchi wa Kata ya Machinjioni katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma-Ujiji mkoani Kigoma, wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko
ikiwemo kipindupindu kufuatia kaya 15 kupoteza vyoo vilivyosombwa na
mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Akizungumza Mwenyekiti wa Mtaa wa Ukumbi, Kata ya Machinjioni, Jumanne
Baheza, amesema mvua hiyo ilinyesha jana majira ya saa 5:00 asubuhi na
kusababisha kaya mbili kubomoka huku vyoo 15 vikisombwa na mafuriko.
Amesema, kusombwa kwa vyoo hivyo kulisababisha kaya 15 kukosa vyoo huku
kukiwa na hofu ya kutanda kwa magonjwa ya mlipuko kwa wakazi wa maeneo hayo
kutokana na uchafu wa vyoo kupelekwa kwenye vyanzo vya maji ambayo wakazi wa
eneo hilo huyatumia.
“Sasa kuna uwezekano mkubwa wa wananchi kupata magonjwa mana kila siku
hutumia maji yanayotoka kwenye vyanzo vya maji (bondeni) ambako ndiko uchafu wa
vyoo ulielekea huko,” amesema Baheza.
Awali katika kikao cha mkoa kilichoketi Novemba 2015 kilichoadhimia
kudhibiti hali ya uchafu katika mkoa huu, Mganga Mkuu wa Kigoma, Leonard Subi
ambaye alisema kuwa Kigoma inakabiliwa na ukosefu wa vyoo bora kwa asilimia
25 na vyoo vingi vimejaa.
Aidha takwimu hiyo ya Mganga mkuu inaonyesha kuwa tatizo la ukosefu
wa vyoo linaongezeka kutokana na athali za mvua zinazoendelea kunyesha mkoani
hapa na kupelekea hofu ya magonjwa ya mlipuko.
Hata hivyo Baheza amewataka wakazi wa kata ya Machinjioni kufuata sheria
na taratibu za afya ikiwa ni kunawa mikono kwa sababuni kabla na baada ya kula
sambamba na kunywa maji yaliyochemshwa pamoja na kuacha tabia ya kuoga
kwenye vyazo vya maji kama alivyoagiza Mganga wa Mkoa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HOFU YA KUENEA KWA KIPINDUPINDU YATANDA KIGOMA”
Post a Comment