Wednesday, January 27, 2016
AMUUA MWENZAKE BAADA YA KUMKUTA AKIMTONGOZA DADA YAKE
Do you like this story?
![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari. |
Mkazi wa kijiji
cha Kalovya – Inyonga wilayani Mlele, Ramadhani Ally (20) amefariki dunia
akipatiwa matibabu hospitalini baada kupigwa na kijana
mwenzake.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari amesema
kuwa Ramadhani alifikwa na umauti baada ya kujeruhiwa na kijana mwenzake Ntema
Kabembenya( 26), mkazi wa kijiji cha Ipwaga.
Kidavashari
amesema tukio hilo lilitokea Januari 22, mwaka huu saa 12:55 jioni ambapo
Ntema alimkuta Ramadhani (marehemu) akimtongoza dada yake (Ntemwa) mwenye umri
wa miaka 12 (jina limehifadhiwa).
“Ntemwa
alikasirishwa na kitendo cha Ramadhani kumtongoza dada yake mwenye umri wa
miaka 12, alimshambulia Ramadhani kwa kumpiga na fimbo na kumjeruhi vibaya,” alieleza Kamanda Kidavashari.
Inadaiwa
Ramadhani alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Mlele kwa matibabu lakini
alifariki dunia siku iliyofuata akiwa anatibiwa.
Kwa mujibu wa
Kidavashari, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo anatarajiwa
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AMUUA MWENZAKE BAADA YA KUMKUTA AKIMTONGOZA DADA YAKE”
Post a Comment