Tuesday, March 15, 2016
AJIBU ASHINDA TUNZO YA MCHEZAJI BORA MWEZI JANUARI 2016 SIMBA SPORT CLUB
Do you like this story?
Ikiwa ni tunzo ya 4 tangu kuanza
kwa zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi ambapo zoezi hili lilianzishwa
mwezi Septemba, 2015 likiwa na dhumuni la kuongeza morali na kuwazawadia
wachezaji wanaofanya vizuri.
Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ameshinda kwa mara ya pili tuzo ya mchezaji
bora mwezi Januari, 2016 baada ya kupigiwa kura kwa wingi na wanachama,
mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za
mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News pamoja na kwenye mitandao
rasmi ya kijamii ya Simba
Facebookwww.facebook.com/simbatanzania Twitter na
Instagram @simbasctanzania.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Rais wa Simba
Evans Aveva amesema, “sisi kama uongozi wa klabu yetu ya Simba tunaamini katika
kuwapa motisha wachezaji wetu kila iitwapo leo na hii ni katika kuongeza chachu
ya maendeleo si tu kwa mchezaji bali kwa klabu nzima kwa ujumla, Ajib anashinda
tunzo hii kwa mara ya pili mfululizo. Wote mtakubaliana nami kuwa kwa kiwango
anachoonesha mshambuliaji Ajib ni kweli mshabiki, wanachama na wapenzi wa Simba
hawajakosea kumchagua tena mchezaji huyu”Napenda kutoa wito kwa wachezaji wetu
wote kuendelea kujituma zaidi kwani mashabiki wao wakiongozwa na uongozi mzima
tunamatumaini makubwa msimu huu 2015/2016, tukiamini kwenye falsafa yetu ya
SIMBA NGUVU MOJA, aliongeza Rais Evans Aveva.
Akizungumza na simbasports.co.tz Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni
washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula amesema,
“EAG Group inapenda kusisitiza kuendelea kuongeza utayari wake katika
kushirikiana na klabu ya Simba kwenye kutoa motisha kwa wachezaji wa Simba
ambapo italeta chachu ya kufanya vizuri zaidi na hivyo kuweza kutengeneza mfumo
mzuri wa kuongeza vyanzo vya mapato na hatimaye faida kubwa kwa wachezaji na
timu kwa ujumla”.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba
habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya
wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba.
Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 kisha utaletewa
ujumbe jibu kwa kutuma neno “OK” na hapo utakuwa umejiunga rasmi, Huduma hii ni
maalum kwa Tigo na Vodacom.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AJIBU ASHINDA TUNZO YA MCHEZAJI BORA MWEZI JANUARI 2016 SIMBA SPORT CLUB”
Post a Comment