Thursday, March 31, 2016
RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI.
Do you like this story?
Rais John
Magufuli amewatoa hofu wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhusu uteuzi wao kwa
kuwataka kuchapa kazi kwa bidii ili wawe na nafasi nzuri ya kuteuliwa badala ya
kufanya kazi kwa wasiwasi jambo ambalo matokeo yake yatakuwa kuondolewa.
Dk Magufuli
alitoa kauli hiyo juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Chato mara baada ya
kutua kwa helikopta akitokea Mwanza kuelekea nyumbani kwake Kijiji cha
Rubambangwe kwa mapumziko.
Akiwahutubia
mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, Dk Magufuli alisema
anatambua kuwa bado hajachagua wakuu wa wilaya na wakurugenzi hali ambayo
imewafanya baadhi yao kuwa na wasiwasi na kushindwa kutekeleza majukumu
inavyotakiwa.
“Kama
wewe ni mchapakazi mkuu wa wilaya, mkurugenzi una wasiwasi gani? Tena unapokuwa
na wasiwasi ndivyo uwezekano wa kung’olewa unakuwa mkubwa,” alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na kuongeza:
“Lazima
niwaambie waheshimiwa wakuu wa wilaya, ukiwa na wasiwasi hutafanya kazi na sisi
tunakuona tu unafanya kazi kwa wasiwasi utaondoka tu kwani wasiwasi ni dalili
nzuri ya kukufanya uondoke.”
Aliwatoa hofu
akisema hata watakaoondolewa kwenye nafasi hizo watapangiwa kazi nyingine
lakini akawaambia kwamba hata kama wataondolewa wasihofu kwani haitakuwa mbaya
kwa kuwa hawakuzaliwa na ukurugenzi au ukuu wa wilaya.
Alisema
Watanzania wanatakiwa kumwamini na kurudia kauli yake kwamba hatawaangusha
akiahidi kuondoa kero ambazo zimegeuka mzigo kwa wananchi.
“Wako
wengine walianza kulalamika natumbua mno majipu, siyo kutumbua tu ikiwezekana
kuna mengine nitayakata kabisa na mguu wake, Tanzania lazima iwe yenye neema,
haiwezekani kuwa na wafanyakazi 5,000 wanaolipwa mishahara mikubwa halafu
Watanzania milioni 50 wanalia… nitakwenda kujibu nini kwa Mungu,” alisema.
Alisema ataendelea
kuwatumbua (kuwawajibisha viongozi wazembe) hata kama wanafika 50,000 ilimradi
Watanzania milioni 50 wapate neema ya kufaidika na rasilimali yao.
Alisema watu
katika nchi hii wanaishi bila raha na kuwaahidi kuwa itapatikana kwa kila mmoja
kufanya kazi kwa bidii hasa vijana na kuacha tabia ya kucheza pool huku mama
zao wakienda shambani kulima na kusubiri kula tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI.”
Post a Comment