Thursday, March 24, 2016
BASATA LATOA ONYO KUMBI ZA STAREHE KUPIGA "DISKO TOTO" KATIKA MSIMU HUU WA PASAKA.
Do you like this story?
Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Godfrey L. Mngereza |
Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki
wote wa kumbi za sherehe na burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika
kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya
Pasaka ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.
Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za
sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida
katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa
ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji
wa kumbi kwa msingi huohuo wa kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya
vibali vyao wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na
BASATA.
BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi
za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote
utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye
kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali
na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.
BASATA linawatakia wasanii na wadau wote
wa Sanaa Pasaka njema na yenye furaha tele.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA
KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA.
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BASATA LATOA ONYO KUMBI ZA STAREHE KUPIGA "DISKO TOTO" KATIKA MSIMU HUU WA PASAKA.”
Post a Comment