Thursday, March 24, 2016
WALINZI WATATU WA SUMA JKT WATIWA MBARONI KWA WIZI WA COMPYUTA 50 CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Do you like this story?
Walinzi watatu
wa Suma JKT na askari mmoja wa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Dodoma,
wametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta zinazokadiriwa kufikia 50 mali
ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom).
Chanzo chetu
cha habari kilieleza kuwa wizi huo ulitokea juzi baada ya chuo hicho kufungwa
kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.
Inadaiwa kuwa
katika wizi huo baadhi ya walinzi wa Suma JKT ambao wanajukumu la kulinda chuo
hicho, walihusika huku watatu wakishikiliwa na polisi.
Hata hivyo,
chanzo hicho kilieleza kuwa baadhi ya askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma
wanadaiwa kuhusika na kuzua mkanganyiko katika uchunguzi wa tukio hilo.
“Katika
wizi huo, pia kuna askari kutoka mjini ametajwa na walinzi wa Suma JKT
kuhusika, sasa baada ya kupata taarifa hizo ndiyo wanafanya mpango wa
kumkamata,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Ofisa Habari wa
Udom, Beatrice Baltazar jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba,
bado hawajajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibiwa.
“Ni
kweli kuna wizi wa kompyuta hapa chuoni, lakini sijajua idadi kamili ya
kompyuta zilizoibwa, ila kuna walinzi watatu wa Suma JKT wanashikiliwa na
polisi kwa mahojiano,” alisema
Beatrice.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa naye alithibitisha kuwapo kwa taarifa
za tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa kuwa yupo
likizo.
Hata hivyo,
Mambosasa alikanusha kuwa hakuna polisi aliyehusika katika tukio hilo bali ni
walinzi wa Suma JKT.
“Hakuna
askari wetu aliyehusika katika tukio hilo, wenye jukumu la kulinda chuo hicho
ni Suma JKT ndiyo wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi,” alisema Mambosasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WALINZI WATATU WA SUMA JKT WATIWA MBARONI KWA WIZI WA COMPYUTA 50 CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)”
Post a Comment