Tuesday, March 15, 2016
ZIJUE FAIDA ZA TIKITIMAJI MWILINI.
Do you like this story?
TIKITImaji
ni miongoni mwa matunda yanayopatikana kwa wingi nchini ni tunda lenye
virutubisho vingi vyenye faida kubwa katika mwili wa binadamu japokuwa asilimia
92 ya tikitimaji huwa ni maji.
Hata hivyo, asilimia 8 zilizobaki zina faida kubwa mwilini jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Tutaeleza baadhi ya faida chache kati ya tikitimaji.
Ndani
ya tunda hili kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia
kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inasaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha,
kukinga uharibifu wa seli, kuboresha afya ya meno na fizi; na vitamini B6,
inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha Protini kuwa nishati.
Tunda
la tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Lycopene kuliko tunda lolote au mboga za
majani.
Ndani ya tunda hili kuna madini ya Potasium. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Tikitimama
pia lina Amino Asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko
wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa
ya kipekee iliyopo katika tunda hili ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza
ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake
iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo
hilo.
Tunda
hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu
mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Kwenye
tikitimaji kuna faida tangu kwenye majani, ganda na tunda na hata nyama yake.
Potassium iliyomo kwenye tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja baada ya kufanya mazoezi, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu, pia husaidia kupunguza uzito mwilini.
Tikitimaji
lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo
kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili linaweza kumsaidia kwa kula kwa
wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana,
hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima
na bila kuathirika kiafya.
Kirutubisho
cha ‘Arginine’ kilichomo kwenye tikitimaji huchochea kwa kiasi kikubwa
uimarishaji wa kinga ya mwili. Huondoa sumu mwilini, vilevile hufanya kazi
muhimu ya uponyaji vidonda na kuondoa ‘Ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo
zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tikitimaji
pia hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu,
huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo
yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya
tumbo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ZIJUE FAIDA ZA TIKITIMAJI MWILINI.”
Post a Comment