Tuesday, March 15, 2016
.RAIS MAGUFULI ATAKA VIJANA WAACHE KUCHEZA POOL TABLE NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI.
Do you like this story?
Rais John
Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na
katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya kuhakikisha vijana
wanafanya kazi na kuacha uzembe.
Rais Magufuli
amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa
wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa
kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.
"Nimeamua
kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa
yenu.
"Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.
"Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana.
"Haiwezekani vijana leo hii unawakuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli

ameongelea pia suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini
ambapo amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna
wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.
"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll
"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll
"Mshahara
wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na
tunampeleka mahakamani
"Singida
na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data
ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila
malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika
kutatua matatizo ya wananchi"
"Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.
"Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani( selo) hata masaa 48,wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa.
"Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.
"Nyinyi mna mamlaka ya kuwaweka watu ndani( selo) hata masaa 48,wekeni watu ndani ili wajue mnatakiwa kuheshimiwa.
"Tusiogope
kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko
mbele."Amesema Rais Magufuli
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “.RAIS MAGUFULI ATAKA VIJANA WAACHE KUCHEZA POOL TABLE NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI.”
Post a Comment