Tuesday, March 15, 2016
DC ARUSHA ATAPELIWA MIL 10 KUPITIA MTANDAO.
Do you like this story?
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkulu akiongea na waaandishi jinsi alivyotapelewa shilingi milioni kumi na wezi wa mitandao. |
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa anaonyesha ujumbe mfupia wa maneno ambao matapeli hao walikuwa wanatuma kwa watu. |
Na
Woinde Shizza, Arusha
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na
wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa
saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa
10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00
usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake
yalitekwa kwa muda.
Mkuu
huyo wa Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye
nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini
juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.
Msaidizi
wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha
kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na
matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta
namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.
Kwa
upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa
kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.
Wizi
wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho
teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za
kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua
hatua kupambana na uhalifu huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DC ARUSHA ATAPELIWA MIL 10 KUPITIA MTANDAO.”
Post a Comment