Thursday, May 19, 2016
AIRTEL NA TFF YAPANGA MIKAKATI YA MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA
Do you like this story?
Dar es Salaam, Jumatano Mei 18 2016 Kampuni ya Airtel
Tanzania leo imekutana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia
mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya
vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka
huu.
Katibu
Mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa ambaye ndio aliongoza kikao hicho, alitoa
shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la vijana ambalo ndio
msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. Naamini ya kwamba kwa kuendelea
kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika mbali kwa kupata matokeo
mazuri.
Tangu
kuanzisha kwa michuano ya Airtel Rising Stars miaka mitano iliyopita, soka la
vijana nchini imekuwa na mafanikio makubwa. Leo, Timu ya Taifa chini ya miaka
20 – Serengeti Boys, imeundwa na vijana ambao wamekuwa ni chimbuko la Airtel
Rising Stars, alisema Mwesigwa na kuongeza kuwa hata timu ya Taifa ya Wanawake
– Twiga Stars, Klabu za Liguu na zile zinazoshiriki ligi daraja ya kwanza,
zinatumia wachezaji ambao wamekuzwa kwa michuano ya Airtel Rising Stars.
Airtel
imeweza kuiwezesha TFF kufika maeneo ambayo yamekuwa ni vigumu kufika kutafuta
vipaji. Kwa kufanya hivyo, tuweza kupata vijana wenye vipaji vingi na hata kwa
sasa hivi, baadhi yao wako na Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti kushiriki
michuano ya Kimataifa inayoendelea India, alisema Mwesigwa.
Katibu
Mkuu huyo wa TFF aliomba Airtel kuendelea kudhamini miradi ya soka ya vijana
kwa vile ndio njia pekee Tanzania inaweza kuwa na timu bora na imara ya Taifa.
Nchi nyingi zinazofanya vizuri kwenye michuano mbali mbali ya soka ni kwa vile
waliweza kuwekeza kwenye program mbali mbali za vijana kama vile Airtel Rising
Stars. Kwa kushirikiana na nyinyi, tutaweza kupata na kukuza vipaja vya soka
ambazo watakuwa na msaada mkubwa kwenye timu ya Taifa.
Kwa
upande wake, Meneja wa Mahusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema
“kampuni yake itaendelea kudhamini program za soka la vijana ambazo zimeweza
kuwa na mafanikio makubwa kwa miaka mitano iliyopita. Lengo letu ni kuwa na
timu ya taifa bora kama vile Misri, Cameron, Nigeria, Ivory Coast na Ghana,
alisema Mmbando huku akisisitiza njia pekee ya kufikia mafanikio hayo ni
kuwekeza na kukuza soka la vijana.
Airtel
pia imetoa shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Michezo na Sanaa
pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushirikiano wao ambao umeifanya
Airtel Rising Stars kuwa moja ya mashindano yenye mafanikio makubwa hapa
Tanzania. Bila ushirikiano na serikali pamoja na wadau wa soka hapa nchini,
Airtel Rising Stars hangeweza kufika hapa ilipo kwa leo, alisema Mmbando.
Mmbando
alisema kwa mwaka huu, Tanzania haitashiriki kwenye michuano ya kimataifa
ambayo huleta pamoja wachezaji waliong’ara kwenye nchi zao Barani Afrika kwa
ajili ya kubadilisha uzoefu, bali itashirikiana na TFF kuweka mikakati
mingi zaidi ya kuwawezesha vijana hawa kufanya vyema hata baada ya mashindano
ya Airtel Rising Stars kwisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AIRTEL NA TFF YAPANGA MIKAKATI YA MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA”
Post a Comment