Tuesday, May 31, 2016
HANS POPPE: HAJAACHWA JUUKO WALA KIIZA, WA KIGENI WOTE BADO WACHEZAJI WA SIMBA.
Do you like this story?
MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba hakuna
mchezaji wa kigeni aliyeachwa hadi sasa na kwamba vyombo vya habari vimekuwa
vikiripoti tofauti.
Akizungumza Hans Poppe amesema kwamba walikuwa wakilalamikia uwajibikaji usioridhisha wa wachezaji wa kigeni wa klabu hiyo, lakini hawakusema wanaachwa.
Akizungumza Hans Poppe amesema kwamba walikuwa wakilalamikia uwajibikaji usioridhisha wa wachezaji wa kigeni wa klabu hiyo, lakini hawakusema wanaachwa.
“Ni kiongozi gani wa Simba alitamka mchezaji fulani kaachwa Simba? Hakuna, hayo ni maneno ya magazeti tu. Sisi tulililalamikia uwajibikaji usioridhisha wa wachezaji wa kigeni, hatujawaachaa,”alisema.
Hans
Poppe amesema kwamba wachezaji wote wenye mikataba na Simba wanaendelea kupewa
stahiki zao kama kawaida wakiwemo hao wa kigeni.
Mwishoni mwa msimu, Simba SC ilitofautiana na wachezaji wake wa kigeni baada ya kugoma kwenda Songea kucheza mechi ya pili kuelekea mwishoni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Majimaji.
Wachezaji hao ni kipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast, mabeki Emery Nimubona kutoka Burundi, Juuko Murshid, kiungo Brian Majwega, mshambuliaji Hamisi Kiiza wote kutoka Uganda na kiungo Justice Majabvi kutoka Zimbabwe ambao waligoma kwa kucheleweshewa kwa wiki moja mishahara ya Aprili.
Hata hivyo, hivyo Simba SC iliwalipa mishahara yao wachezaji hao na kuteua wawili, Angban na Majabvi kwenda Songea siku moja kabla ya mechi.
Kilichofuatia hapo ni habari za magazeti kwamba Simba SC itaacha wachezaji wote wa kigeni na kusajili wapya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HANS POPPE: HAJAACHWA JUUKO WALA KIIZA, WA KIGENI WOTE BADO WACHEZAJI WA SIMBA.”
Post a Comment