Tuesday, May 31, 2016
MKE WA TRAFIKI KINYOGORI ADAIWA KUKIRI KUMUUA MUMEWE
Do you like this story?
MKE wa
askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki), Sajenti Ally Salum
(Kinyogori) aliyeuawa hivi karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji
hayo, akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke mwingine.
Kamanda wa
Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa
habari jana kuwa mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo
yaliyofanyika nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani.
Wakati huo
huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya Anathe Msuya yaliyofanyika hivi
karibuni Kigamboni na kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za
nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha mwanamke huyo.
Anayetuhumiwa
kuua mumewe
Akizungumza
na waandishi wa habari jana kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza
jijini Dar es Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa Kinyogori
amekiri kuhusika.
Kwa mujibu
wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake kwa sababu za
kipelelezi, aliamua kumtuma mtu kutekeleza mauaji hayo baada ya mumewe kumwacha
na kuoa mke mwingine.
“Ni
jambo la kusikitisha kuona mtu anatoa uhai wa mtu sababu ya kuachwa. Tunawasihi
wananchi kuepuka kujihusisha na matukio kama haya, eti sababu tu ya kuachwa
wanawake wapo wengi na wanaume wapo wengi unaweza kuachwa na ukaolewa na ukaoa
kuliko kuondoa uhai wa mtu,”
alisisitiza Sirro.
Hata
hivyo, Sirro alisema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili waweze kuwataja
watu wengine walioshirikiana nao kutekeleza tukio hilo baada ya kuonekana
kuwepo kwa wahusika wengine.
‘Hausigeli’
asakwa
Kuhusu
mauaji ya Anathe aliyechinjwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni, Kamanda Sirro
alisema wanaendelea na jitihada za kumtafuta msichana huyo ahojiwe kuhusu tukio
hilo.
Aidha
alisema mtu mmoja anashikiliwa akituhumiwa kuhusika na tukio hilo huku polisi
ikiwa imeandaa timu ya upelelezi itakayoshughulikia tukio hilo kufanikisha
kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.
Sirro
alisema msichana huyo aliondoka siku moja kabla ya tukio hilo la mauaji hivyo
kupatikana kwake, kunaweza kusaidia polisi kujua kama kuondoka kwake kulikuwa
salama au kuna kitu kimejificha.
“Msichana
huyu tunaendelea kumsaka tujue kama aliondoka salama na kumhoji zaidi juu ya
kuondoka kwake siku moja tu, tukio linatokea nina imani tutafanikiwa kumpata na
wote waliohusika na kukomesha matukio haya,”
alisema Sirro.
Mamia
wajitokeza msibani
Vilio na
simanzi jana vilitawala wakati mamia ya wakazi wa Kibada Kigamboni na Salasala
walipokuwa wakiuaga mwili wa marehemu Anathe Msuya (30), aliyeuawa Mei 25
nyumbani kwake kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.
Mwili
ulichukuliwa jana asubuhi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa
nyumbani kwake Kibada, kwa ajili ya kuagwa na majirani zake kabla ya
kusafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Arusha leo.
Akizungumza
baada ya mamia kumuaga nyumbani kwa marehemu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Nyakwale Kibada, Said Pazi alisema kuwa wao kama majirani waliomba familia
wapate fursa ya kumuaga jirani yao ambaye tangu ahamie ana muda wa miezi sita.
“Baada
ya kuambiwa msiba upo Salasala tuliomba kama majirani na sisi tupatiwe fursa ya
kuuaga mwili wa ndugu yetu ambaye alihamia mwaka jana… kwa kweli msiba wake
umetusikitisha sana” alisema.
Akizungumzia
tukio hilo alisema kuwa mtoto wa marehemu huyo, Allan Kimario (4) aliwataarifu
majirani kuwa mama yake haamki na ndipo walipofika wakakuta ameuawa.
Mwenyekiti
huyo alitoa pole na kusema atahakikisha wanaimarisha ulinzi na kuhimiza wenye
viwanja ambavyo havijajengwa, wavifanyie usafi ili kuondoa vichaka ambavyo ni
hatari kwa usalama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKE WA TRAFIKI KINYOGORI ADAIWA KUKIRI KUMUUA MUMEWE”
Post a Comment