Tuesday, May 31, 2016
WABUNGE WA UPINZANI WAMETOKA NJE YA BUNGE KUONYESHAKUTOKUWA NA IMANI NA SPIKA TULIA ACKSON
Do you like this story?
Wabunge wa
vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk.
Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Taarifa kutoka
Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha
Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.
Baada tu
ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha
Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.
Hata hivyo
Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani
hawamwamini tena.
Wameeleza
kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia
haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea
kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.
Kutokana
na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.
Mbowe aliwaambia
hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na
kushirikisha waandishi wa habari.
Alisema,
Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa
Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.
“Nitapendekeza
kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili
kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.
Utekelezwaji
wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM
pekee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WABUNGE WA UPINZANI WAMETOKA NJE YA BUNGE KUONYESHAKUTOKUWA NA IMANI NA SPIKA TULIA ACKSON”
Post a Comment