Wednesday, May 18, 2016

HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO.


Baadhi ya nyaraka zilizoungua katika afisi hiyo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Kitabu cha hundi kilicho hathiriwa na Moto.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)



Msaidizi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Dr Agnes Buchwa akizungumza mara Baada ya Moto huo kutokea.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


HOSPITALI ya Mkoa wa Mbeya,  imenusurika kuteketea kwa moto baada ya chumba kimoja cha ofisi ya uhasibu inayotumiwa na Taasisi binafsi ya Walter Reed kushika moto na kuteketeza mali zote zilizomo ndani ya ofisi hiyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Justus Kamugisha, alisema moto huo ulitokea juzi majira ya saa mbili asubuhi, ambapo chumba kimoja cha ofisi ya uhasibu kilishika moto na kuteketeza vitu vyote vilivyomo ndani zikiwemo nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na ofisi hiyo.

Aidha, katika tukio hilo Polisi Mkoani Mbeya, linawashikilia baadhi ya watu akiwemo muhasibu wa Taasisi hiyo ya Walter Reed, Samweli Mwakyusa kwa ajili ya mahojiano.

“Mbali na watu hawa kuhojiwa pia, polisi wanalichunguza tukio zima kwani tayari yameibuka mambo mengi katika tukio hilo na zaidi yamekuwa yakihusishwa na hujuma Fulani hivyo ni kazi yetu sisi kuchunguza na kuzitolea taarifa,”alisema

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu wa hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Agnes Buchwa, alisema kuwa Taasisi hiyo ya Walter Reed, imekuwa ikiisaidia hospitahiyo kwa kutoa fedha za huduma za afya.

“Kutokana na kuhudumia huduma hizo, taasisi ilikuwa inatumia chumba kimoja cha ofisi kwa ajili ya usimamizi wa fedha zao za mradi  ambazo zilikuwa chini ya muhasibu Samweli,”alisema.

Hata hivyo, kiongozi huyo alisema  majira ya saa mbili asubuhi wakiwa ofisini walishangaa kuona moshi mkubwa ukitoka ndani ya ofisi hiyo na hivyo kuwahi kutoa taarifa katika kitengo cha zimamoto ambao walifika kwa haraka na kudhibiti motoi huo usisambae kwenye maeneo mengine jambo ambalo lilifanikiwa.

Hata hivyo, alisema katika tukio hilo hakuna madhara makubwa ya binadamu yaliyotokea isipokuwa ni kuungua kwa vifaa kama vile compyuta  na nyaraka mbalimbali zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya hospitali hiyo.
Mwisho.

0 Responses to “HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA YANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO.”

Post a Comment

More to Read