Wednesday, May 25, 2016
MBEYA CITY HAKUNA KULALA, YAANZA KUSAKA NYOTA WAPYA
Do you like this story?
SIKU
chache baada ya pazia la ligi kuu ya soka Tanzania bara
kufungwa,Kocha mkuu wa Mbeya City FC Kinnah Phiri ameanza zoezi
maalumu la kusaka nyota wapya ambao atawajumuisha moja kwa moja kwenye
vikosi vya timu yake msimu ujao.
Akizungumza
muda mfupi baada ya majaribio ya siku ya kwanza kwa wachezaji wapya
vijana waliofika kujaribu bahati zao kwa kuonyesha vipaji walivyonavyo
navyo, afisa habari wa City Dismas Ten amesema kuwa muitikio umekuwa mzuri
katika siku hii kwanza ambayo nyota hao wa baadae wamefika kuonysha uwezo
wao mbele ya kocha huyo raia wa malawi.
ni
siku ya kwanza, kitu kizuri mwitikio umekuwa mkubwa, takribani vijana 50
wamejitokeza kujaribu bahati zao kulingana na vipaji walivyonavyo, haya
ni majaribio ambayo kocha Phiri ameyaitisha ili kusaka vipaji vipya ambavyo
moja kwa moja vitaingia kwenye timu yetu kubwa na ile ya U20, alisema.
Akiendelea
zaidi, Ten alisema kuwa, hii imekuwa ni kawaida kwa City kila
inapofika mwisho wa msimu kuwaleta pamoja vijana wote wanaoamini
wanauwezo wa kucheza mpira, kufichua vipaji vyao ili waje kuwa wachezaji
wakubwa baadae.
“Hii
ni kawaida yetu, kila tunapomaliza msimu huwa tunafanya hivyi, vijana wote
wenye umri kuanzia miaka 17-22 ni fursa kwao kujitokeza, zoezi hili la kusaka
vipaji litakuwepo kwa juma zima, leo hatukuwa na kocha Phiri kwa sababu
alikuwa kwenye majukumu mengine lakini kesho tutakuwa kwenye uwanja
Sokoine na mwalimu atakuwa, kwa hiyo vijana wote ndani ya jiji la Mbeya
na mikoa ya jirani waje kujaribu bahati zao.
Kwa
upande wa vijana waliojitokeza siku ya leo, walishukuru kuwepo kwa zoezi hili
kwa sababu limerahisisha uwezekano wa vipaji walivyonavyo kuonekana
mapema hatimaye waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji wakubwa siku
za usoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY HAKUNA KULALA, YAANZA KUSAKA NYOTA WAPYA”
Post a Comment