Monday, May 23, 2016

UCHAMBUZI WA JOSE MOURINHO KWA NAMBA.




Jose Mourinho ni kama tayari vile amemalizana na Manchester United isipokuwa ni suala la wakati kufika na kutangazwa tu kuwa kocha mpya wa ‘Mashetani Wekundu’.

Licha ya Van Gaal kuwapa United kombe la FA, lakini hakufanikisha kuleta furaha ile ambayo mashabiki na viongozi wa klabu hiyo walitaraji kuipata kama ambavyo walikuwa wakipata katika utawala wa Sir Alex Ferguson.

Van Gaal hana tayari ameshafungashiwa virago na nafasi yake itachukuliwa na Mreno huyo mwenye maneno na mbwembwe nyingi.

Van Gaal amejitilia ugumu mwenyewe kutokana na kushindwa kuipa ndoo ya EPL United, lakini vile vile kushindwa kuipa nafasi ya kucheza michuano ya UEFA mwakani kitu ambacho kimekuwa ni fedheha kubwa kwa mashabiki hasa ukizingatia historia, umaarufu na ukubwa iliyonayo klabu yao.

Uvumilivu umeonekana kuwashinda na sasa wanaamua kumkabidhi mikoba Mourinho ambaye mara zote amekuwa ni kocha wa makombe tu. Ikumbukwe kuwa Mourinho alishawahi kufanya kazi chini ya Van Gaal akiwa kocha msaidizi wakati huo akikinoa kikosi cha FC Barcelona mwishoni mwa miaka ya 90.

Hivyo basi, kuelekea uteuzi wa Mourinho kuwa kocha mkuu wa Manchester United, tunakuletea uchambuzi juu ya Jose Mourinho kwa njia ya namba.

1 – Katika masiha yake ya soka akiwa nchini England akikinoa kikosi cha Chelsea, Mourinho amewahi kufungwa mara moja tu na Manchester United katika michezo ya ligi kuu nchini humo. Mourinho amepoteza mara moja tu dhidi ya United katika kipindi chote alichodumu nchini England kama kocha wa Chelsea.
5 – Makombe mengine aliyowahi kuchukua akiwa ligi kuu England akiwa na Chelsea – makombe matatu ya ligi, Kombe la FA moja, na Ngao ya Jamii moja.

6 – Idadi ya timu alizowahi kufundisha, alianza na Benfica mwaka 2000. Nyingine ni Uniao de Leiria, Porto, Chelsea (alifundisha kwa vipindi viwili tofauti), Inter Milan na Real Madrid.

Mourinho alichukua makombe matatu (treble) ndani ya msimu mmoja wakati akiifundisha timu ya Inter
9 – Vipigo ambavyo Chelsea ya Mourinho ilivipata katika michezo 16 ya mwanzo ya EPL msimu huu, jambo lililopelekea kutimuliwa kwake. Mourinho alitimuliwa December mwaka jana kutokana na mfululizo wa matokeo mabovu.

32 – idadi ya makombe aliyochukua, yakiwemo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mawili, makombe matatu ya Ligi Kuu England, Makombe mawili ya ligi ya Serie A, La Liga moja na ubingwa wa Ligi Kuu ya Ureno mara mbili. Mourinho amebeba ndoo 32 katika maisha yake ya soka
87 – Pointi ambazo Mourinho alifikisha wakati akiwapa Chelsea ubingwa wa EPL msimu wa 2014-15. Lakini miezi saba baadaye akafukuzwa.
513 – idadi ya michezo ya ligi ambayo ame-manage akiwa kwenye vilabu sita alivyowahi kufundisha.

0 Responses to “UCHAMBUZI WA JOSE MOURINHO KWA NAMBA.”

Post a Comment

More to Read