Monday, May 23, 2016
MKENYA AFUNGA NDOA NA MWANAMME MWENZAKE MMAREKANI.
Do you like this story?
Bw. Ben Gitau na Bw. Steve Damelin. |
KATIKA
matukio ambayo wanaume wa Kenya wanaoana na wanaume wenzao katika nchi
zinazoruhusu jambo hilo, mwanamme mmoja wa Nakuru, Kenya, amefunga ndoa na
profesa wa hisabati wa Marekani.
Bw.
Ben Gitau (33) na Bw. Steve Damelin walioana wiki iliyopita huko Ann Arbor,
Michigan, Marekani, Jumamosi alasiri ambapo baada ya tukio hilo wawili hao
walionekana wakibusiana na kukumbatiana ambapo marafiki na wanafamilia walipiga
vigelegele na kushangilia.
Hata
hivyo, mshauri mmoja wa masuala ya kifamilia , Mchungaji Philip Kitoto wa
International Christian Centre, Nairobi,alilaani ndoa hiyo akisema:
“Kiutamaduni na kwa mujibu wa Bibilia, ndoa na kujamiiana kati ya watu wa
jinsia moja ni dhambi.”
“Biblia
iko wazi kwamba Mungu alituumba kwa taswira yake; mme na mke. Katika
kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22 Mungu anamwonya mwanaume kutofanya ngono
na mwanaume mwenzake kama anavyofanya na mwanamke.”
Bw.
Kararu Ririe, rafiki wa karibu wa wanandoa huyo ambaye ni Mkenya
aliyewahi kukiri kwamba ni shoga anayeishi California, Marekani, alitume ujumbe
kwenye mtandao wa twitter baada ya ndoa hiyo akiandika kwamba: “Jioni hii
nilimpongeza rafiki yangu, Ben na mumewe Steve, kwa ndoa yao. Ni jambo
adimu kwa Mkenya kuwa jasiri kiasi hicho. Hongera.”
Gitau
alikuwa anaishi Atlanta, Georgia, kabla ya kuhamia California. Kwa mujibu
wa mwanafamilia mmoja aliyezungumza na gazeti la Daily Nation, Gitau
alikutana na mchumba wake huko Atlanta ambako Damelin alikuwa mwanafunzi wa
shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo cha Teknolojia cha Georgia.
Katika
kulaani tukio hilo, Mchungaji Kitoto alisisitiza kwamba tendo la ndoa
kati ya mwanamme na mwanamke liliwekwa kwa ajili ya uzazi.
Ndoa
za jinsia moja zilihalalishwa katika Jimbo la Michigan mwaka jana mwezi Julai na
Mahakama Kuu ya Marekani iliyoondoa sheria zinazopinga ndoa za watu wa jinsia
moja mradi tu wawe wanapendana.
Source:
Daily Nation
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKENYA AFUNGA NDOA NA MWANAMME MWENZAKE MMAREKANI.”
Post a Comment