Monday, May 23, 2016
TAZAMA MADIWANI WA JIMBO LA MISUNGWI WAIBUKA NA KUMTETEA CHARLES KITWANGA
Do you like this story?
Mtendaji wa kampuni ya CZ Information & Media Consultant Ltd, Bw. Cyprian Musiba akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kwa niaba ya Madiwani juu ya kumtetea Charles Kitwanga. |
UTANGULIZI
Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano
huu mfupi ambao lengo lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha
kuhusu kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi
wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.
Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari,
taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa.
UFAFANUZI
Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais
Dk John Pombe Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo
ya Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la kwamba
Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa.
Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa
sana na taarifa na uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika
iliyopelekea Mhe Rais kufanya maamuzi haya. Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango
wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi ukilenga kumchonganisha Mbunge
wetu na Mhe. Raisi uliopangwa na waovu wachache ambao wamebanwa na Serikali hii
ya Awamu ya tano kupitia wizara hiyo nyeti kwa usalama wa nchi.
Itakumbukwa kuwa, Mhe Charles kitwanga alinadiwa na
Mhe Rais na wanaCCM na baadae kupigiwa kura kwa wingi na wananchi wa Misungwi
kwa ajili ya uwezo wake na dhamira yake njema ya kulinda taifa letu. Sisi
wananchi wake, tunaamini katika uwexo wake, uadilifu wake na nidhamu ya kazi
aliyonayo, hatuna mashaka na hili.
Baada ya kuteuliwa na Mhe Raisi kama Waziri wa mambo
ya ndani, amekuwa muadilifu na kafanya mengi katika kuimarisha usalama na
kufanya maamuzi yengi mazuri kwa maslahi ya taifa. Hili lilimtengenezea maadui
wengi ndani ya serikali, ndani na nje ya CCM, mtandao wa dawa za kulevya,
walioachishwa kazi NIDA na Uhamiaji. Watu hawa ndio waliochochea na kutengeneza
mkakati wa kumchafua Mhe Kitwanga na walikuja dodoma kuhakikisha dhamira yao
ovu inatimia.
USHAHIDI WETU
Miongoni mwetu tulikuwa mjini Dodoma pamoja na
madiwani wa Jimbo la Misungwi ambao tulikwenda kumtembelea Mbunge wetu bungeni,
tulizungumza mengi kwa ajli ya jimbo letu na katika kikao chetu hapakuwa na
chembe ya kilevi chochote na hata kesho yake alipoinga bungeni alikuwa mzima wa
afya ya kimwili na akili timamu na tunawahakikishieni kuwa Kitwanga hakuwa
amelewa.
Ndugu waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 20
tulielekea bungeni kwa mwaliko wa Charles Kitwanga, tukiwa sehemu ya mualiko
uliowajumuisha Madiwani wa jimbo lake tukiwa tumeambatana naye tukaingia ndani
ya ukumbi wa bunge,tukashuhudia anajibu swali,baada ya kujibu swali la mbunge
Sakaya,tulitoka nje na kupiga picha na madiwani wote wa Misungwi waliokuja
kumtembelea Dodoma.
Baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika pale nje
ya ukumbi wa Bunge, tulitoka na kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo
la kututembeza maeneo yote ya Dodoma , lakini ilipofika jioni wakati
tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa kwenye
mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa kuwa alionekana
na Waziri Mkuu akiwa amelewa.
Ndugu wanahabari , tulishangazwa wote kwani
tulikuwa tumekaa naye pale nyumbani kwake Dodoma (site 2) tukipata chakula cha
usiku ,alionekana kutoaamini na hata madiwani pia na wengine ambao tulikuwepo
hapa nyumbani kwake hatukuamini.
Tunachosema ni kwamba waziri Kitwanga hakulewa kama
ambavyo imepotoshwa, bali alikuwa ni mkakati wa kumchafua na kuhakikisha
andavuliwa wadhifa wake ili watu hawa waendelee kufanya maovu yao.
Mtandao wa dawa za kulevya, pamoja na wale waliokuwa wanamshutumu kwamba
amehusika kuondolewa kwao kazini wakiwemo Watu wa NIDA, Mbunge wa Jimbo la
Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mfanyabiashara Said Lugumi pamoja na
kundi mafisadi waliokwapua mabilioni ya fedha NSSF.
Pia na baadhi
ya wabunge wa CCM na Upinzani ambao walikuwa hawafurahishwi na kasi ya utendaji
kazi wa Kitwanga katika Wizara ya Mambo ya ndani.
Kwa niaba ya wananchi wenzetu tunamuomba na
kumtahadharisha Mhe. Rais awe makini na makundi la wafanyabiashara wa madawa ya
kulevya, pamoja na lile kundi la wanamtandao masalia ndani ya CCM na
serikalini na kwenye vyombo nyeti vya ulinzi na usalama, ambayo kwa ujumla
yalikuwa na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamtenganisha na kumpotosha Mhe
Raisin a kumjaza habari zisizo za kweli.
Ndugu waandishi wa habari, kilichotushangaza zaidi
baada tu ya Kitwanga kuvuliwa madaraka yake ya uwaziri, kuna watu walianza
kufanya sherehe wakishangilia hususani wale waliovuliwa madaraka NIDA pamoja na
NSSF,Uhamiaji na wale wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.
Ndugu waandishi wa habari, tunajua namna kundi la
Said Lugumi, Ridhiwani Kikwete na kampuni yao walivyokuwa wanadhamini kwa
mbinu za kifedha katika vita hii ya kitwanga ili aondolewe, lakini baada
ya kuondolewa, wakajifanya kutoa taarifa ya kushangazwa kuondolewa kwake,
Kitwanga amekuwa mtumishi wa serikali akiwa mtumishi
mwandamizi benki kuu Tanzania (BOT),amekuwa mbunge na Naibu waziri kwa miaka
10,lakini hata siku moja hakuwahi kuonekana amelewa. Ni muadilifu na ana
nidhamu ya kazi, na nidhamu hii ndiyo iliyomfanya aaminiwe na kupewa dhamana
hii.
MAAZIMIO YETU
=Tunaliomba Bunge kumuomba radhi Mhe. Charles
Kitwanga kwa kumdharirisha mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Misungwi
familia yake pamoja na watanzania wote waliokuwa wanaamini utendaji wake kupitia
video iliyochezewa na wataalamu wa IT katika studio za Bunge ili kufanikisha
lengo la kumuonyesha Kitwanga kuwa alikuwa amelewa bungeni.
=Tunamuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye
ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali bungeni atoe uthibitisho wa kikemia
unaotanabaisha wazi kama Kitwanga alikuwa katumia kilevi wakati
akiwa bungeni maana hakuna kipimo chochote kilichofanyika kudhibitisha uvumi
huu.
=Tunaliomba Bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale
wote walisambaza ile video inayoonyesha Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana
amelewa wakati kiuhalisia hakulewa na alijibu maswali yote vizuri
=Tunaliomba Bunge kuchunguza idara ya habari ya
Bunge pamoja na studio ile ya Bunge ambao wamehusika na kuhariri ile picha ya
video iliyokuwa inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
=Tunahoji uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu
ya ulevi bila uthibitisho wa daktari ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo
kugundua kilevi cha mtu.
= Tunaomba Watanzania wote waliosikitishwa na
taarifa hizi wajue tu kwamba ile video ambayo imemtia hatiani Kitwanga
ilihaririwa kwa ustadi mkubwa kupitia wafanyakazi wa Bunge ambao wanapitia zile
asadi za bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya
ulinzi na usalama ambao hawakupenda kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya
kumhujumu na sasa wanasema kwenye vyombo vya habari ili kuhalalisha uhujumu
huo.
=Tunaomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)
kuangalia picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge
wa Misungwi ambazo zinaonekana kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao kwani
kisiasa zinaendelea kumchafua na kumharibia kwa wapigakura wake,familia
yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .
=Tunajiandaa kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria
kama watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Charles Kitwanga ambazo
tunaamini zimetengenezwa kwa maslahi ya makundi yanayompinga ndani ya Serikali
wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.
Pia tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuwa makini kundi la wanamtandao walio ndani ya serikali ambalo
linaongozwa wahafidhina wasio taka mabadiliko ndani ya serikali .
Imeandaliwa na madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja
na wakereketwa wa jimbo hilo.
Baraka Kingamkono,Gaudency Tungaraza na IDDY
Majumuisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ TAZAMA MADIWANI WA JIMBO LA MISUNGWI WAIBUKA NA KUMTETEA CHARLES KITWANGA”
Post a Comment