Monday, May 23, 2016
WATANZANIA KUANZA KUNUFAIKA NA HATI FUNGANIYA NMB
Do you like this story?
- Wateja na wasio wateja wa NMB kunufaika kwa Kiwango cha uwekezaji cha kuanzia Kiwango TZS 500,000
- Hati fungani ya NMB inapatikana katika matawi yote ya NMB na kwa mawakala.
Benki ya NMB PLC imeanza kutoa hati
fungani ya NMB yenye riba ya 13% kwa yeyote mwenye nia ya kuwekeza na kupata
faida nzuri.
Hii ni mara ya kwanza kwa NMB kutoa
hati fungani ya namna hii na inaweza kununuliwa kupitia matawi yote ya NMB au
kwa mawakala wanaotambulika kwa kiasi cha chini cha shilingi 500,000 (laki tano
tu).
Kufunguliwa kwa hati fungani ya NMB
kwa wananchi ni matokeo ya kupata kibali kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji
nchini - Capital Markets & Securities Authority (CMSA).
Wawekezaki wa hati fungani ya NMB
watapata riba ya asilimia 13 kwa mwaka itakayolipwa kila baada ya miezi sita
kwa miaka mitatu mpaka mwezi Juni 2019; Riba itakayotolewa itakatwa kodi ya
mapato.
Hati fungani ya NMB inauzika pia, na
mteja anaweza kuiuza kwa mnunuaji mwingine na kupata fedha yake kabla ya
kmukomaa kwa hati fungani – yaani miaka mitatu.
Wawekezaji wanaweza kuiuza hati
fungani hiyo kabla ya kukomaa katika soko la wazi kupitia mawakala wa soko la
mitaji – kwa kufuata misingi ya soko la hisa la Dar es Salaam.
Hati fungani ya NMB itauzwa kuanzia
tarehe 10 Mei, 2016 mpaka June 8 2016 na riba itaanza kulimbikizwa kuanzia
tarehe hii. Kununua hati fungani ya NMB, mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote
la NMB kati ya matawi 175 nchini kote au kwa mawakala wanaotambuliwa.
Tembelea tawi na NMB kunua hati
fungani hii na hakikisha umebeba viambatanishi vifuatavyo;
- Fomu ya bondi iliyokamilika na kusainiwa
- Nakala ya kitambulisho
- Akaunti ya CDS
- Kianzio cha fedha cha shilingi 500,000
- Taarifa za akaunti yako ya benki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATANZANIA KUANZA KUNUFAIKA NA HATI FUNGANIYA NMB”
Post a Comment