Sunday, May 29, 2016
WANAFUNZI 7,000 WATIMULIWA UDOM
Do you like this story?
Chuo Kikuu
cha Dodoma (Udom) kimewasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi
maalumu ya ualimu wa sayansi kwa ngazi ya stashahada na kuwataka waondoke
chuoni hapo mara moja.
Jana,
lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya jana
hadi leo saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo
yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea
majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.
Makamu
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula alipotakiwa kufafanua suala hilo,
alisema kwa ufupi kuwa suala hilo lipo lakini akaelekeza apigiwe simu Ofisa
Uhusiano wa chuo hicho, Beatrice Baltazal kwa maelezo zaidi.
Baltazal
alipotafutwa alisema kusimamishwa kwa wanafunzi hao kulitokana na agizo la
Serikali na wametakiwa kulitekeleza.
Kuhusu
lini na nini hatima ya wanafunzi hao, alisema bado hawajui hadi hapo
watakapoelekezwa vinginevyo.
Hata
hivyo, kulikuwa na malalamiko kwa wanafunzi hao juu ya namna walivyopewa
taarifa za kusimamishwa masomo yao kwa ghafla na kutakiwa kuondoka.
Kozi ya
stashahada ya ualimu wa sayansi, ilianzishwa maalumu kwa agizo la Rais Jakaya
Kikwete kwa lengo la kuziba pengo la walimu wa sayansi na ilikuwa inatolewa
UDOM pekee.
Waliokuwa
na sifa za kujiunga na kupewa mikopo ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na
kufaulu vizuri masomo ya sayansi.
Wanafunzi
hao waliokuwa wamekopeshwa na Serikali wamesimamishwa siku mbili baada ya
wenzao zaidi ya 480 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph kusimamishwa baada ya
kubainika hawakuwa na sifa za kudahiliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WANAFUNZI 7,000 WATIMULIWA UDOM”
Post a Comment