Saturday, June 4, 2016
BONDIA NGULI WA MAREKANI MUHAMMED ALI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 74
Do you like this story?
Bingwa wa zamani wa ndondi na mwanaharakati wa nchini Marekani, Muhammad Ali ‘The Greatest’ amefariki dunia.
Ali alifariki Ijumaa hii kwenye hospitali ya huko Phoenix ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya kupumua.
Alikuwa na umri wa miaka 74.
“After a 32-year battle with Parkinson’s disease, Muhammad
Ali has passed away at the age of 74. The three-time World
Heavyweight Champion boxer died this evening,” Bob
Gunnell, msemaji wa familia aliiambia NBC News.
Ali has passed away at the age of 74. The three-time World
Heavyweight Champion boxer died this evening,” Bob
Gunnell, msemaji wa familia aliiambia NBC News.
Taratibu za mazishi zinafanyika kwenye mji wake wa Louisville, Kentucky.
Bondia huyo alizaliwa kwa jina la Cassius Marcellus Clay Jan. 17,
1942 huko Louisville, Kentucky. Alianza kucheza ndondi akiwa na miaka 12
na kushinda mikanda kadhaa kabla ya mwaka 1960 kushiriki mashindano ya
Olympic mjini Rome, na kushinda medali ya dhahabu. Muda mfupi baadaye
aliingia kwenye ndondi za kulipwa.
Akiwa amekuwa maarufu Ali alianza kupambana na ubaguzi wa rangi
nchini Marekani. Baada ya kukataliwa kupewa huduma kwenye duka la soda,
alisema aliitupa medali yake ya dhahabu ya Olympic mtoni.
Akiwa na miaka 22, alilikataa jina la Cassius Clay kwa kudai ni la
kitumwa na kuanza kujiita Muhammad Ali. Mwaka 1967, wakati wa vita vya
vietnam alikataa kulitumikia jeshi la Marekani kwa madai kuwa vita hivyo
havikuendana na msimamo wa dini yake.
Kutokana na uamuzi huo, alinyang’anywa mkanda wake na kuhukumiwa
kifungo cha miaka mitano jela. Aliachiwa baada ya kukata rufaa lakini
akazuiwa kupigana au kuondoka nchini.
Baada ya kupewa tena kibali cha kupigana alimshinda Jerry Quarry na
miezi sita baadaye kwenye pambano lililopewa jina ‘pambano la karne’ na
kuchukua round 15, Ali alishindwa kwa mara ya kwanza na Joe Frazier.
Ali na Frazier walipigana tena mwaka 1974. Ali alishinda.
Alikuja kuuchukua mkanda wa ubingwa wa dunia kwa kumpiga George
Foreman baadaye mwaka huo kwenye pambano lililopewa jina “The Rumble in
the Jungle,” na kufanyika Zaire.
Ali alikuja kupigana tena na Frazier mara ya tatu katika pambano la
mwaka 1975, “Thrilla in Manila” ambalo hadi sasa linaaminika kuwa
pambano bora zaidi katika muda wote.
Ali aliendelea kuutetea mkanda wake hadi mwaka 1978, alipopigwa na Leon Spinks, na kisha kuuchukua tena.
Alistaafu mwaka 1979, alipokuwa na miaka 37 lakini akarudi tena mwaka
1980 na kupambana na Larry Holmes na kushindwa. Ali alishindwa tena na
Trevor Berbick, mwaka uliofuata na ndipo alipoamua kustaafu kimoja.
Bondia huyo alifunga ndoa mara tatu na zote zikavunjika huku akipata watoto tisa akiwemo Laila, aliyekuja kuwa bondia pia.
Ali alimuoa mke wake wa mwisho, Yolanda “Lonnie” Williams mwaka 1986; na
wameishi kwa muda mrefu huko Berrien Springs, Michigan, kisha kuhamia
Arizona.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BONDIA NGULI WA MAREKANI MUHAMMED ALI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 74”
Post a Comment