Friday, June 3, 2016

MICHAEL JORDAN AUNGANA NA NEYMAR KUTENGENEZA VIATU VIPYA VYA NIKE







Staa wa soka wa timu ya Barcelona, Neymar na legend wa mchezo wa kikapu duniani, Michael Jordan wameungana kutengeneza viatu vipya vya soka vya ushirikiano wa Nike/Jordan.

Mshambuliaji huyo wa Brazil anakuwa mcheza soka wa kwanza kuhusishwa kwenye viatu vya Jordan.

Namba 23 aliyokuwa akiitumia Jordan enzi zake ni maarufu nyuma ya viatu hivyo pamoja namba 10, namba anayovaa Neymar anapoichezea timu yake ya taifa.

Wawili hao waliamua kufanya kazi pamoja kutengeneza kiatu kipya kutokana na kuheshimiana kwao kwa mafanikio waliyoyapata kwenye michezo yao.

Viatu hivyo viitwavyo Jordan V vitatoka vikiwa na jina la Neymar kwenye ulimi wake.

Neymar ameandika herufi za jina la mwanae, DL (David Lucca) na bendera ya Brazil kwenye viatu hivyo.

‘I’m excited that Neymar and the Jordan Brand are working together. ‘I’m a fan of his creativity, style and passion for the game of soccer. He’s a special player and I look forward to this collaboration,” alisema Jordan.

Naye Neymar aliongeza: ‘Michael Jordan set the standard for greatness. He’s an incredible competitor and a champion. I’ve always admired him, so to collaborate with him and have his icon on my boots means a great deal to me.’

Neymar, ambaye kwa sasa yupo likizo Marekani, atavivaa viatu hivyo kwenye michuano ya Olimpiki mwaka huu.

Viatu hivyo vinavyouzwa kwa $190 vimeanza kupatikana leo June 3 kupitia Nike.com.

0 Responses to “ MICHAEL JORDAN AUNGANA NA NEYMAR KUTENGENEZA VIATU VIPYA VYA NIKE”

Post a Comment

More to Read