Thursday, June 30, 2016
WABUNGE WATATU WA CHADEMA WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE
Do you like this story?
Mbunge wa Mbeya
mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Joseph
Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya Bunge kuanzi leo kufuatia
kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.
Joseph Mbilinyi
alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kile
alichoeleza kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake. Hata hivyo
alipohojiwa kama anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi alisema kuwa hamfahamu.
Hukumu hiyo
imesomwa leo na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson baada ya Mwenyekiti wa
Kamati ya Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati hiyo ilijiridhisha kuwa kitendo
kilichofanywa na mbunge huyo kuwa ni kosa.
Aidha wabunge
wangine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge ni pamoja na Saed Kubenea,
Mbunge wa Ubungo, James Ole Millya Mbunge wa Simanjiro kwa makosa
yanayofanana ya kusema uongo bungeni. Wabunge hawa wamesimamishwa kuhudhuria
vikao vitano kuanzi leo.
Katika hatua
nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha mkutano wa tatu wa Bunge
lililokuwa na lengo la kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka wa
fedha 2016 2017. Kufuatia kuahirishwa huko, kuanzia kesho Julai Mosi, serikali
itaanza kutekeleza miradi na mpango mingine iliyoanishwa katika bajeti hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WABUNGE WATATU WA CHADEMA WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE”
Post a Comment