Monday, July 25, 2016
AFISA TAKUKURU AFARIKI KIFO CHA UTATA.
Do you like this story?
Jeshi
la Polisi Mkoa Manyara limeripoti kutokea kwa kifo cha afisa mmoja wa TAKUKURU Bi Evanjelina Samson
Mahili (39) kwa kudhaniwa kupigwa na
kitu kizito (butu) Nyumbani kwake mtaa wa Bomani kata ya Kibaya Wilayani kiteto
Akizungumza
na Fahari News kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara ACP Akili Mpwapwa amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kwamba Jeshi la Polisi Mkoani hapo lina washikiria watu wa 4 kwa
uchunguzi zaidi
Kamanda
Mpwapwa amesema kuwa uchunguzi wa awali
uliofanywa na Jeshi la Polisi unaonesha kuwa maarehemu kabla ya kukutwa na
umauti alikuwa akipata chakula cha jioni na na mtu ambae bado hakufahamika kwa
kukuta sahni mbili za chakula mezani nyumbani kwa marehemu
Awali
majira ya saa kumi na moja marehemu alionekana maeneo ya Baa akiwa
anakunywa na mmoja kati ya watuhumiwa
wanne wanashikiliwa na na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi,
Tukio
hilo la kustahajabisha lilitokea usiku wa kuamkia Jumanne ya tarehe 19 mwezi
Julai mwaka huu majira ya usiku.
Aidha
kamanda Mpwapwa ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kuwataka
wawe watulivu katika kipindi hiki ambacho jeshi la Polisi likifanya uchunguzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AFISA TAKUKURU AFARIKI KIFO CHA UTATA.”
Post a Comment