Sunday, July 17, 2016
AU YAZINDUA CHETI CHA KUSAFIRIA
Do you like this story?
Hivi
Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !
Kisa
na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!
Madhumuni
ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na
mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Viongozi
wa kiafrika wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda katika kongamano
la viongozi wa Afrika.
Wakwanza
kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya
kidiplomasia.
Viongozi
wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa
Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.
Marais
wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa cheti hicho cha AU kabla ya
kukamilika kwa mkutano huo.
Mawaziri
wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa
kufaidi cheti hicho cha kusafiria.
Umoja
wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya
vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ AU YAZINDUA CHETI CHA KUSAFIRIA”
Post a Comment