Sunday, July 17, 2016
KINARA WA MAPINDUZI UTURUKI AKAMATWA
Do you like this story?
Jenerali Erdal Ozturk (katikati) aliyekuwa kinara wa jaribio akiwa mikononi mwa wananchi. |
Jenerali
Erdal Ozturk aliyekuwa kinara wa jaribio lililoshindikana la mapinduzi ya rais
nchini Uturuki amekamatwa, huku viongozi wengine wa mapinduzi hayo saba
wakifanikiwa kutoroka na kukimbilia nchi jirani ya Uturuki kwa kutumia
Helikopta.
Hata
hivyo viongozi hao waliokimbilia nchini Uturuki wakiwemo mameja wawili,
makapteni watano na raia mmoja wamekamatwa nchini humo kwa kile kilichoripotiwa
kuingia nchini humo bila kibali.
Jenerali
Erdal Ozturk aliyekuwa kamanda mkuu wa kikosi namba tatu tayari amekamatwa na
kuwekwa mahabusu wakati akisubiri hatma yake na huenda akanyongwa ikiwa
atapatikana na hatia hiyo.
Mapinduzi hayo yalishindikana baada ya wananchi wengi kujitokeza kumsapoti Rais Recep Erdogan, ambaye ametamka bayana kwamba wote waliohusika na jaribio hilo lililoshindikana watakabiliwa na adhabu ya kifo.
Katika jaribio hilo imeripotiwa raia 161 wamefariki, 1,440 wamepata majeraha makubwa, na wastani wanajeshi 2,9000 wamekamatwa wakiwemo majenerali wawili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KINARA WA MAPINDUZI UTURUKI AKAMATWA”
Post a Comment